''Wacheza bao, wavaa kobasi waliokuwa na ilmu akhera'' na wasifu wa Julius Nyerere

''Wacheza bao, wavaa kobasi waliokuwa na ilmu akhera'' na wasifu wa Julius Nyerere

Mohamed Said, kati ya hao wazee wa Dar-es-salaam, naomba unitajie walioteuliwa kushika nyazifa za kiserikali Tangu Uhuru, Jamuhuri hadi Muungano.

Maana kama walikuwa kipaumbele kwenye kupigania uhuru bila shaka walikumbukwa kwenye nyazifa nyeti za serikali ya wakati huo. La sivyo watakuwa walimkaribisha Nyerere awaongoze tu.

Pia mwandishi wa kitabu cha UWIKE USIWIKE KUTAKUCHWA kuna ajenda gani aliyofanya kitabu chake kipigwe ban.

Mwisho kwenye historia ya uhuru wa Tanganyika. Je kuna mtu anaitwa Martin Kayamba.

Naomba unijuze hayo tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
Mega...
Swali umeliuliza sivyo.

Kwanza Baraza la Wazee wa TANU halikuwa pale kudai uhuru ili ukipatikane wapate kazi.

Pili wao siyo waliomchagua Nyerere.

Vipi Nyerere aliingia katika uongozi wa TAA Makao Makuu ni historia nyingine kabisa.

Unaweza kusoma historia ya Martin Kayamba katika kitabu cha Iliffe (Ed)"Modern Tanzanians (1973).

Kayamba kafa miaka ya 1940.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati lazima ukubali kwamba nyerere alikuwa na elimu kubwa au upeo mkubwa kuwashinda hao wapigania Uhuru wenzake ndio maana aliwatumia kama ngazi kisha aka wa-dump

Hayo haya kuwa makosa ya nyerere kwa sababu katika siasa na maisha mwenye elimu au upeo mkubwa humtumia mwenye upeo Mdogo ili kuweza kufikia malengo yake ... So hayo ni matatizo yao wenyewe maana walishindwa kuchanga karata zao vyema nakutambua kwamba nyerere anawatumia kama ngazi .... Kwa namna 1 ama nyingine tunaweza kusema kwamba hao wazee upeo wao kwa wakati huo haukuwa toshelezi

Sent using Jamii Forums mobile app
1 . Rais wa AA Cecil Matola mgalatia
2 . Rais wa TAA Dr Kyaruzi mgalatia
3 . Rais wa TANU Dr Mwl Nyerere mgalatia

Sasa ukiniambia Wagalatia hawakuwa mstari wa mbele kudai uhuru wakati viongozi Wakuu wote walikuwa Wagalatia nabaki nashangaa na kusikitika.

Historia ya Tanganyika kama inavyosimuliwa na Sheckh Mohamed Said katika kile kitabu chake cha kumuenzi Babu yake hakina maana wala huwezi kusema ndio historia ya Tanganyika.
 
Ngongo,
Ndiyo faida ya kuandika na ukasomwa na watu.

Kila msomaji atasoma kitu kile kile lakini kila mmoja ataelewa kadri ya maajaliwa ya kichwa chake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 . Rais wa AA Cecil Matola mgalatia
2 . Rais wa TAA Dr Kyaruzi mgalatia
3 . Rais wa TANU Dr Mwl Nyerere mgalatia

Sasa ukiniambia Wagalatia hawakuwa mstari wa mbele kudai uhuru wakati viongozi Wakuu wote walikuwa Wagalatia nabaki nashangaa na kusikitika.

Historia ya Tanganyika kama inavyosimuliwa na Sheckh Mohamed Said katika kile kitabu chake cha kumuenzi Babu yake hakina maana wala huwezi kusema ndio historia ya Tanganyika.
Wewe sijui upo dunia ya wapi? Umeelewa lakini alichoandika mwandishi?
 
Wewe ndio haujaelewa msome tena na tena Ustadhi Mohamed utamwelewa.
Ngongo,
Unatonesha kidonda mimi si ustadh lau kama natamani kama ningekuwa.

Kuna jamaa wengi huniita Profesa, Dk. na huwaleza kuwa sikujaaliwa kiwango cha elimu hiyo.

Wananichoma moyo wangu kwani ningependa niwe.

Sasa wewe unaniongezea ilm nyingine ambayo sina.

Unauchoma moyo wangu.
 
Back
Top Bottom