Wachezaji 10 wa kigeni uwanjani sio sawa

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Mpira wa miguu ni ajira mbali ya kuleta furaha na sifa kwa vilabu, mashabiki na taifa. Ligi kuu ina timu 16 na kama timu itaweza kusajili wachezi 10 wa kigeni maana yake wageni 160 watashiriki ligi kuu nchini. Kama kocha akiamua kuwapanga wachezaji wote 10 uwanjani, maana yake mzawa mmoja tu ndiye atakaepata nafasi ya kucheza kwenye mechi hiyo. Tunaelekea wapi? au ni njia ya kuzibeba timu kubwa zenye wafadhili wenye hela?
 
sio timu zote zinaweza kusajili wachezaji 10 wa kigeni.
Halafu wazawa nao wajitume au watoke waende nje kucheza sio kung;ang'ania hapo kariakoo
kwahiyo hiyo kanuni ni kwaajili ya Simba tu kisa yuko mo mwenye hela ya kusajili? tff bwana kuna mambo, wanaibadilishia goal post timu moja.
 
Ngoja tuone mwisho wake nini kitatokea mana tangu timu fulani kupata nguvu za kiuchumi kanuni na sheria zina badilika kuwa sapoti ila wakumbuke udhamini wa timu za tanzania sambamba na uongozi ni suala la muda tu sasa sijui wataendelea na magumashi yao maana sasa viongozi wamekuwa hawa angalii mustakabali wa mpira wa tanzania bali wanaelekeza mapenzi kwenye vilabu wana vyo vipenda.
 
Simba ni malimbukeni Sana, hivi ukiwa na wachezaji 10 wa kigeni kwenye klab halafu wote wakaitwa kwenye timu zao za taifa klabu itabakiwa na nini? Na vipi kama mfadhiri akabwaga manyanya ghafla mishahara Yao itatoka wapi?

Ndio sababu wamelikosa Kagame Kwa unafiki
 
sio timu zote zinaweza kusajili wachezaji 10 wa kigeni.
Halafu wazawa nao wajitume au watoke waende nje kucheza sio kung;ang'ania hapo kariakoo

Mmewatengeneza kuweza kumudu kucheza nje...sio kazi rahisi kaka.
 
sio timu zote zinaweza kusajili wachezaji 10 wa kigeni.
Halafu wazawa nao wajitume au watoke waende nje kucheza sio kung;ang'ania hapo kariakoo
England timu zao zimejaa wazawa lakini ni waingereza wangapi wanacheza nje ya England, timu Yao ya taifa ina ubora gani duniani?
 
England timu zao zimejaa wazawa lakini ni waingereza wangapi wanacheza nje ya England, timu Yao ya taifa ina ubora gani duniani?
Kuweka kikomo cha wachezaji hakisaidii timu ya taifa kiivyo. Kuwabeba wachezaji bila kua na sifa haisaidii timu ya taifa. Ngoja tujaribu hii labda itawasaidia wachezaju wetu kujituma maana tumewabeba sana lakini hatujaona chochote kwenye timu ya taifa
 
England timu zao zimejaa wazawa lakini ni waingereza wangapi wanacheza nje ya England, timu Yao ya taifa ina ubora gani duniani?
Timu ya taifa ya England ina ubora.
Katika kombe la dunia linaloendelea imeshika nafasi ya Nne.
 
Binafsi sijaipenda hii sijui wamefikiria nini,huku ni kulididimiza soka la nchi yetu.

Wachezaji saba walitosha kabisa uamuzi huu uliofikiwa niwakukurupuka.
 
Hii safi sana. Kama wazawa wana ‘akili’ itawamotivate sana kupambana. Uchache wa wachezaji wa kigeni haukuzi soka letu,zaidi linafanya wazawa kuwa wazembe wazembe tu.

Tufanye tathmini fupi tu,toka tumeanza na wakigeni kuwa wa 3 tukaja 5,soka letu hasa ngazi ya kimataifa limepiga hatua gani? Na vipi hao wazawa waliokuwa wanawakilisha vilabu vyao kimataifa kipi walichokifanya zaidi ya kuonekana wabovu hasa kwa kukosa uzoefu?!
Cha umuhimu,timu zisajili kweli wachezaji wa kimataifa ili kuleta tija kwenye soka letu na sio janjajanja.
Bravo TFF kwa hili.
 
Wakati soka letu lilipokuwa juu enzi za akina Mzee Bendera rip klabu zetu hazikuwa na wageni. Uganda, Rwanda, Burundi hakuna wageni wengi lakini viwango vyao vya soka viko juu kuliko Sisi.
 
Hizi timu hazijui tu,wachezaji wa ndani wana mpira mzuri sana kuliko hao wa nje,muangalie Kichuya,Bocco,huyu dogo wa Azam Shabaan Idd,Manula,Salamba,dogo aliotoka Mbao kwenda Singida hlf njoo kwa hawa international pros Chirwa,Papii, nk
 
Inaelekea Mo kuidhamini Simba imekuuma sana mkuu??[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hilo ndio tatizo let...tunawabeba baadala ya kuwaa daa. Tukiwaandaa wataweza kupambana na wageni lakini tatizo let someone nyingiii bila utekelezaji.
 
Wakati soka letu lilipokuwa juu enzi za akina Mzee Bendera rip klabu zetu hazikuwa na wageni. Uganda, Rwanda, Burundi hakuna wageni wengi lakini viwango vyao vya soka viko juu kuliko Sisi.
Kikubwa ‘Mentality’ mkuu. Hata mshahara haukuwepo hiyo zamani ila timu zilipambana kufanya vyema,umejiuliza kwanini sasa hivi tunatoka patupu?. Vijana wanataka pesa nyingi halafu kazi hawapigi ipasavyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…