Mwenzetu mmoja kauwawa akiwa anaenda dukani, mwingine mtaani kwetu kauwawa siku ya Alhamisi, kulikuwepo joto Dar akatoka kwenda kujaribu kutafuta maji mchana kweupe akapogwa risasi barabara ya wazi kabisa mtaani.
Mwingine aliacha hela kwenye kiduka chake cha kuuza pombe, akaenda Jumatano kufungua ili kuchukua hela akapate mahitaji maana uchumi wa Dar raia wengi wanakula hela waliyopata siku hiyo au iliyolala jana, akauwawa.
Na bado hatujazungumzia kesi za waliopotea, wasiojulikana wako wapi kuanzia hiyo Jumatano, Alhamisi na Ijumaa kila siku walikuwa wanapotea watu kadhaa.