Wachezaji Argentina wagoma kupeana mikono na Trump

Wachezaji Argentina wagoma kupeana mikono na Trump

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,914
Reaction score
168,320
NYOTA wawili wa timu ya soka ya Taifa ya Argentina, Lisandro Martinez na Cristian Romero, walionekana wakikwepa kupeana mikono na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Ni wakati wa kukabidhiwa medali ya kufika fainali ya msimu huu wa Kombe la Dunia, ambapo Argentina walikosa ubingwa baada ya kufungwa bao 1-0.

Baada ya mchezo, kama ilivyo kawaida, mgeni rasmi, Rais Trump, alitakiwa kuwavalisha medali wachezaji wa timu zote, akianza na Argentina.

Baada ya Martinez ‘kupotezea’ mkono wa Rais Trump, Romero naye alifanya hivyo, kisha kuwasalimia Rais wa Mexico, Claudia Sheinbaum, na Waziri Mkuu wa Canada, Mark Carney.

Tukio hilo linakuja wakati Rais Trump akiendelea kutokuungwa mkono kwa sera zake, ambapo fainali za mwaka huu zikiahuhudia baadhi ya wachezaji, viongozi na mashabiki wakizuiwa kuingia Marekani.


 
Hata wachezaji waliompa mkono Trump unaona kabisa hawakua friendly kama ambavyo walifanya kwa wale wengine pale jukwaani. Halafu trump alivyokua kichaa akalazimisha atokee kwenye picha ya spain ya ubingwa 😀😀😀. Infantino akajaribu kumtoa. Trump akakataa
 

Ronaldo, you are the greatest of all time. We need you in America. Get going, we need you fast,” Trump posted on social media.
Alisema wapi
Akija kukuonesha Trump aliposema hivyo mimi hydroxo nitakuonesha mkojo wa sisimizi.
 
Back
Top Bottom