Wachezaji Bora hawawezi kubadili uraia ili kucheza Taifa Stars

Wachezaji Bora hawawezi kubadili uraia ili kucheza Taifa Stars

ngara23

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2019
Posts
9,091
Reaction score
21,087
Acha na vigezo vingine kutoka FIFA

Wachezaji wanaobadili uraia ni makapi yaliyotemwa Africa Magharibi ambao hata hawatambuliki kama wanafanya kazi ya kucheza mpira labda mataifa Yao wanajua ni vibarua tu

Kwa mfano

1.Azizi ki - Burkina Faso
Huyo hata umpe mbuga ya Serengeti, hawezi kukubali kuvaa jezi ya Stars aache kuchezea Burkina Faso, yenye platform kubwa

2. Dijui Diara - Mali
Goal Keeper namba 1 wa Mali hawezi kubadili uraia ili atumike huku kwetu

3. Aucho- Uganda
Captain wa team ya Taifa ya Uganda ambayo ndo timu Bora ukanda wa CECAFA aje kubadili utaifa kucheza mavumbini huku, never

4 Pacome Zouzou - Ivory Coast
Mchezaji anayeitwa timu yenye mastaa kama akina Frankie Kessi, Adingira, Sebastian Haller aje kuvaa jezi ya Taifa stars never

5 Max Mpia Nzengeli
Mchezaji aliyecheza DRC aje kurubuniwa kuwa Mtanzania ili acheze Taifa stars, never

6. Ngoma - DRC
CV ya Ngoma ni kubwa na ana heshima kubwa kwao DRC hawezi kukubali kubadili uraia ili acheze stars

7 Camara pin 📌 📍
Goal Keeper wa kwanza kwenye Kikosi cha Guinea hata umhonge bandari hachezi stars

8 Valentine Nouma
Mchezaji anayecheza timu ya Taifa ya Burkina Faso hawezi kukubali kubadili uraia ili acheze Stars

9 Clatous Chama_ Zambia
Yaani mchezaji mwenye heshima huko Zambia aje acheze Stars, hilo haliwezekana

10 Prince Dube
Striker tegemezi timu ya Taifa Zimbabwe hawezi kubadili uraia ili atumike huku kwetu

Hao watawashawishi akina Mukwala, Chamou, Mutale,Debora, Okajepha na magalasa mengine
 
Ni ubadhirifu tu umwefanywa na yule jamaa wa fedha kuwapa hao magalasa uraia
 
Si nimesikia kuwa kwa sheria za sasa za FIFA ni mpaka baada ya miaka mitano ndio mchezaji anaruhusiwa kuchezea nchi aliyochukua uraia. Kama ni kweli basi hao wakina Ugali wa Bada, Yekeyeke na Ngumbaro tutawatumia Taifa Stars mwaka 2030 sasa sijui wao watakuwa na miaka mingapi wakati huo.

Sisi walalahoi tunahimizwa tulipe tozo na kodi mbali mbali huku wajanja wanatoa uraia kirahisi kwa wachezaji ili wasiwalipie kodi, vibali na tozo mbali mbali. Hivi huu sio ukwepaji wa kodi kijanja kweli?
 
Back
Top Bottom