Wachezaji gani walistahili kutwaa Ballon D'or?

Mwaka 2010 hadi Leo cjaamini kwamba Andres Iniesta hakuchukua hyo tuzo akaishia kupata Messi. Ili na wewe ushangae jaribu kucheki mafanikio yao kwa mwaka huo. Na iniesta alifunga bao hadi siku ya final ya world cup mwaka huo.

Na kuna mwaka hapa Africa Adebayo alipewa uchezaji bora Wa Africa kwa sababu alikuwa mfungaji bora ktk timu ya Arsenal hapo haikuchukua ubingwa, wakati opponent wake mmoja wapo alikuwa Mohammed Aboutrika akiwa Captain Wa Al Ahly, aliiongoza timu hyo kutwaa kombe LA klabu bingwa Africa, akiwa captain tena Wa timu ya taifa mwaka huo huo akaiongoza timu hyo kutwaa ubingwa Wa Africa na alikuwa mfungaji bora Wa mashindano. Mwenye kukumbuka vema mwaka na kisa hicho anikumbushe zaidi, mana niliumia sana.
 
Requelme iniesta Xavi robben and ustazi ribbery.

Messi ni bora kwa miaka 10 mfululizo,cha ajabu ana 5!! na kama wangelikuwa wanafuata performance basi Messi mpaka sasa angekuwa na nyingi sana akifuatiwa na iniesta and xavi...
 
Ballon d or ya msimu wa kombe la dunia mara nyingi huamuliwa na perfomance za kombe la dunia..kwa hyo tusubiri


# still messi is better than ronaldo#
 
Kwa miaka ya karibuni naona FIFA wanataka kutuaminisha kuwa ili uwe mchezaji bora ni lazima uwe na magoli mengi. Labda tusubir messi na ronaldo wapite huenda tuzo zitarudia hali yake.

Je hiyo ni haki?
 
2010 - Sneijder
2012 - Iniesta
2013 - Ribery
2014 - Lahm / Neuer
 
Requelme iniesta Xavi robben and ustazi ribbery.

Messi ni bora kwa miaka 10 mfululizo,cha ajabu ana 5!! na kama wangelikuwa wanafuata performance basi Messi mpaka sasa angekuwa na nyingi sana akifuatiwa na iniesta and xavi...
ni kweli usemacho ila kuna watu walikuwa bora zaidi yake kwa miaka hiyo 10
 
Messi hafai kabisa, wamatumbi huku wanateseka kwa sababu yako, wengine mpaka wanazimia na kupata maradhi yasiyotibika. Messi wahurumie hawa viumbe wenye chuki na husda dhidi yako inatosha sasa....miaka 11 kwenye ubora wako sio mchezo,wakati hakuna mchezaji yeyote alifikia hayo mafanikio....
 
Ribery, Ronaldo, Iniesta, Neuer, Xavi, Sneijder, Robben

katika hiyo miaka 10 kuna baadhi Messi alipotea na hao niliyowataja walikuwa/waliwasha zaidi yake

Hahahaaa imebidi nicheke tu, yani messi umlinganishe na hao!!!, ebu kuwa muwazi basi kamanda, hao wote ulowataja sio kweli....alafu nataka uniambie mwaka upi messi alidrop? Maana kuna kipindi aliumia na akakaa nje miezi kibao, na alivyorudi alikiwasha kama kawaida yake....


Wachambuzi wa soka waliobobea wanaujuwa mpira zaidi yangu mimi na wewe, na wamekiri kuwa Messi amekuwa bora kwa 10 mfululizo na huu wa 11,kitu ambacho hakijawahi kutokea kwa mchezaji yeyote ulimwenguni, sasa wewe kama nani ubishe!!! Si utaonekana wa ajabu kamanda....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…