Wachezaji Simba sc waahidiwa mil 10 kila mchezaji wakishinda mechi ya marudiano

By Dick Dauda - March 8, 2018.

Baada ya Simba SC kutoka sare ya kufungana ya bao 2 kwa 2 dhidi ya Al Masry ya Misri, Tajiri wa klabu hiyo
amefanya kikao cha siri na wachezaji wa Simba SC.

Kikao hiko ambacho kilifanyika masaa machache baada ya kumalizika kwa mtanange huo hapa jijini Dar es salaam. Kilikuwa kinajumuisha
wachezaji wote wa klabu hiyo huku ikiwatenga baadha ya viongozi wakuu wa benchi la Ufundi. Tajiri huyo wa Simba SC alioneka
kuwa na mshawasha wa kuifanikisha klabu hiyo kuweza kufika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha muda mrefu.

Aliwataka wachezaji waweze kujitolea kwa kila hali kwenye mchezo ujao wa marudiano na kuwaahidi kuwa endapo wakiweza kupata ushindi wa
namna yeyote ambao utawawezesha kutinga hatua ya makundi basi kila mchezaji wa klabu hiyo atazawadiwa kiasi cha shilingi milioni 10.

"Ni kweli tumeahidiwa kiasi cha milioni 10 kwa kila mchezaji, tutaenda kufanya kila liwezekanalo licha ya kuwa mpira una matokeo matatu." Alisema mmoja
wa mchezaji wa Simba SC aliyekuwamo kwenye kikao hiko huku akiomba jina lake lisiwekwe hadharani.

Nikiwa kama ' Mtaalam ' wa Saikolojia ya Mawasiliano na kwa jinsi ninavyowajua Wachezaji hasa wa Kitanzania walivyo ukiachia wale wachache wa Kigeni huyo aliyetoa hiyo ahadi ajue ndiyo ameharibu kabisa kwani hivi sasa ' concentration ' ya Wachezaji haiko tena katika Kujiandaa na huo mchezo wa marudiano bali sasa najua kila mmoja anawaza ataenda Kulewa wapi, atatafuta Demu gani mkali, atanunua Gari gani, atanunua Nguo gani ili kushindana na akina Messi na Ronaldo. Ila nina uhakika pia tena wa 100% kuwa hata huyo aliyetoa hiyo ahadi ni kama vile ' amewasanifu ' tu kwani anajua fika kuwa Safari ya Simba SC katika CAF CC ndiyo imemalizikia juzi pale Uwanja wa Taifa baada ya kutoka Sare ya 2 kwa 2 na katika hili wala tusidanganyane au kujipa moyo. Kiushabiki Simba SC itafuzu mechi ya marudiano ila Kiufundi kabisa GENTAMYCINE nasema Simba SC tumeshatoka na kilichotokea Dar es Salaam juzi ni Msiba na maziko ya ' Marehemu ' wetu tunaenda kuyafanyia nchini Misri wiki ijayo.
 
By Dick Dauda - March 8, 2018.

Baada ya Simba SC kutoka sare ya kufungana ya bao 2 kwa 2 dhidi ya Al Masry ya Misri, Tajiri wa klabu hiyo
amefanya kikao cha siri na wachezaji wa Simba SC.

Kikao hiko ambacho kilifanyika masaa machache baada ya kumalizika kwa mtanange huo hapa jijini Dar es salaam. Kilikuwa kinajumuisha
wachezaji wote wa klabu hiyo huku ikiwatenga baadha ya viongozi wakuu wa benchi la Ufundi. Tajiri huyo wa Simba SC alioneka
kuwa na mshawasha wa kuifanikisha klabu hiyo kuweza kufika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha muda mrefu.

Aliwataka wachezaji waweze kujitolea kwa kila hali kwenye mchezo ujao wa marudiano na kuwaahidi kuwa endapo wakiweza kupata ushindi wa
namna yeyote ambao utawawezesha kutinga hatua ya makundi basi kila mchezaji wa klabu hiyo atazawadiwa kiasi cha shilingi milioni 10.

"Ni kweli tumeahidiwa kiasi cha milioni 10 kwa kila mchezaji, tutaenda kufanya kila liwezekanalo licha ya kuwa mpira una matokeo matatu." Alisema mmoja
wa mchezaji wa Simba SC aliyekuwamo kwenye kikao hiko huku akiomba jina lake lisiwekwe hadharani.
shithole.
 
Hahaaaa si anajua kabisa watapigwa hamsa!
 
Hata waahidiwe ndege hawawezi kushinda! Mwaka 1993 dhidi ya kina Bolizozo waliahidiwa gari aina ya KIA bado walishindwa tena hapa hapa shamba la bibi!
Usinikumbushe ya Stella Abdijan,
Ile mechi wanadai Azim Dewji alieahidi KIA kila mchezaji aliwageuka Simba kisiri siri
 
Ha ha ha! nadhan hata huyu aliyewaahid M 10 atawageuka tu! Mwaka ule wakiwa na watu kama Masatu, Masha na Mwameja walichezea 2, sembusa hawa kina mlipili
 
Bora wasingeahidiwa,,, wanaenda kupigwa nyingi sana. Al masry sio wa mchezo mchezo.....waarabu wanaujua mpira bwana.
 
Ha ha ha! nadhan hata huyu aliyewaahid M 10 atawageuka tu! Mwaka ule wakiwa na watu kama Masatu, Masha na Mwameja walichezea 2, sembusa hawa kina mlipili

Wanaenda kufumuliwa na wenye mpira wao. Sisi twendelee kula ugali na rosti ya mapanki 😀😀😀
 
By Dick Dauda - March 8, 2018.

Baada ya Simba SC kutoka sare ya kufungana ya bao 2 kwa 2 dhidi ya Al Masry ya Misri, Tajiri wa klabu hiyo
amefanya kikao cha siri na wachezaji wa Simba SC.

Kikao hiko ambacho kilifanyika masaa machache baada ya kumalizika kwa mtanange huo hapa jijini Dar es salaam. Kilikuwa kinajumuisha
wachezaji wote wa klabu hiyo huku ikiwatenga baadha ya viongozi wakuu wa benchi la Ufundi. Tajiri huyo wa Simba SC alioneka
kuwa na mshawasha wa kuifanikisha klabu hiyo kuweza kufika hatua ya makundi kwa mara ya kwanza baada ya kipindi cha muda mrefu.

Aliwataka wachezaji waweze kujitolea kwa kila hali kwenye mchezo ujao wa marudiano na kuwaahidi kuwa endapo wakiweza kupata ushindi wa
namna yeyote ambao utawawezesha kutinga hatua ya makundi basi kila mchezaji wa klabu hiyo atazawadiwa kiasi cha shilingi milioni 10.

"Ni kweli tumeahidiwa kiasi cha milioni 10 kwa kila mchezaji, tutaenda kufanya kila liwezekanalo licha ya kuwa mpira una matokeo matatu." Alisema mmoja
wa mchezaji wa Simba SC aliyekuwamo kwenye kikao hiko huku akiomba jina lake lisiwekwe hadharani.
Ndo ujue kitu ambacho hakiwezekani mtu atoe zaidi ya M 200 kwasasa siamini
 
Wachezaji wetu hawana lishe bora unategemeaje matokeo chanya uwanjani
 
Back
Top Bottom