Wachezaji Taifa star wanadai posho zao

Labda ndio maana kulikuwa na Harambee ya kuchangia timu ya Taifa

Harambee zishakuea nyingi, timu za vijana, timu ya wanawake mara yanga na sasa timu ya Taifa. Hizi harambee hazitakiwi kufanywa kitu cha kawaida ndio maana hatupati hela za maana zinazoeleka. Hebu fikiria ukubwa wa timu ya Yanga na jinai walitangaza Harambee mwezi mzima lakini hata Bil 1 hawakufika.
 
Bora wagome Tu haina namna pesa zao zimetumbuliwa Kwa kununulia wabunge na madiwani wa upinzani huku wao wakiambuliwa kupanda ndege Tu.
Mechi ya Kesho achieni magoli kama 10 hivi ili aibu wapate viongozi wa ccm
 
Warudi nyumbani. Mbona mwenzao bondia alikwenda kupigana huko nje kabla ngumi hazijaanza akanyoosha mikono kuwa ameshindwa. Kuna haja gani kupigana wakati unajua utapigwa? Nilimshangaa waziri Mwaki akisema eti afungiwe. Yeye anaweza kupigana ngumi?
 
Heheheeee wazee wa kubet washayaona mapeeeema haya mambo na ndio maana katika kila mechi ya Starz watakayocheza, wao wamebet starz inakufa........
Wanajua fika wachezaji wetu hawajalipwa so wajitume ili iweje
 

Hao Wachezaji wa Timu ya Taifa Stars, Kocha wao Amunike ambaye namchukia mpaka basi kwakuwa hafai na hatufai pia pamoja na TFF hadi Wizara husika wasitake kutufanya Watanzania wote ni Majuha. Ukweli ni kwamba wameshajua kuwa Makapu ya Magoli tunaenda Kurudi nayo kutoka huko nchini Misri hivyo sasa wanatujenga Kisaikolojia ili hata wakifanya huko vibaya basi Kisingizio kikuwa kiwe Wachezaji waligoma, michango haikutosha na kwamba Serikali iliwatenga.

Ni Mwendawazimu tu pekee ndiyo atadhani kuwa Taifa Stars itazifungwa Timu za Senegal, Algeria na Kenya ambazo itakabiliana nazo. Kitu pekee ninachokijua na nina uhakika nacho kama Taifa Stars hii ya Kocha Mbovu na Mbinafsi itatoka huko na Alama ( Point ) basi ni 1 moja ila nina uhakika wa 100% kuwa Taifa Stars itamaliza huko ikiwa na Alama ( Point ) Sifuri ( Zero ) kabisa.

Kocha mwenye Akili na anayejua vyema Mpira kamwe hawezi Kuwaacha Wachezaji wazuri, tegemeo na muhimu kama akina Mkude, Ajib, Chilunda, Banda na Kichuya huku akifanya pia Kosa kubwa mno la Kumuacha ( Kumuondoa ) Kikosini Mchezaji Kinda kabisa Kelvin John ambaye nina uhakika angekuwepo tu huko hata kama asingempanga Kwake Yeye ( Kelvin John ) ingekuwa ni exposure ya Kutosha ambayo ingemjenga na kumsaidia pia hata Kisaikolojia na baadae ndiyo angekuja kuwa Mbadala mzuri mno wa Nahodha Mbwana Ally Samatta Kikosini.

Kama kuna Mtanzania ambaye anaiombea mabaya Taifa Stars ifungwe basi ni Mimi na mtanisamehe sana kwa hili.
 
nasikia Kelvin John anatakiwa na TP Mazembe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…