Wachezaji wa kibongo hawatakiwi huko nje au?

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
Kumekuwa na wimbi kubwa la wachezaji kutoka pande zote za bara la Afrika (kaskazini, Mashariki, Magharibi, Kati, Kusini) kuingia katika ligi yetu hasa vilabu mbalimbali hapa nchini.

Hivi hawa wa kwetu na wao kwanini hawatoki gumu ndani waende wakapambane huko nje?

Najua tatizo haliwezi kuwa lugha maana hata hawa mapro wengi tu lugha kwao ni changamoto lakini wanatawala soka la hapa ndani.

Sasa tatizo ni uwepo wa mawakala au nini hasa au wachezaji wenyewe hawajielewi au kujiamini?
 
Nje kama wapi?! Ulaya au hapahapa Africa?

Kama ni Africa umefanya utafiti kujua ni wangapi wanaocheza ligi za Africa?

The same to Ulaya ni wangapi?
 
Nje kama wapi?! Ulaya au hapahapa Africa!? Kama ni Africa umefanya utafiti kujua ni wangapi wanaocheza ligi za Africa?! The same to Ulaya ni wangapi?
hilo la kutafiti nalo mkuu? hukuona ile aibu ya afcon kocha anaokotaokota wachezaji ilimradi tu kaambiwa huyo ana asili ya ktz kumbe wengine hata kuongea tu kiswahili full chenga
 
Ukiacha Shabalala, baka, na Feisal nimchezaji gani wa ligi ya bongo anayeweza kucheza Soka la kulipwa nje?
 
Ukiacha Shabalala, baka, na Feisal nimchezaji gani wa ligi ya bongo anayeweza kucheza Soka la kulipwa nje?
Shabalala na Feisal hata Yanga tu hawawezi pata namba, huko nje nani atawasajili?
 
Ukiacha Shabalala, baka, na Feisal nimchezaji gani wa ligi ya bongo anayeweza kucheza Soka la kulipwa nje?
naamani watakuwepo tu mkuu na wengine wanaweza wanaweza kuwa madaraja mengine ya chini lakini wazuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…