Wachezaji wa kigeni waliotamba ligi kuu ya bongo

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
18,960
Reaction score
67,654
Tumeshuhudia utitiri mkubwa wa wachezaji wa kigeni wakija hapa kwetu kucheza ligi yetu. Wengi wao huwa ni magarasa lakini wachache huwa ni wachezaji haswa.

Ni wachezaji gani wa kigeni uliwahi kuwakubali hasa baada ya kutamba katika ligi yetu ya Bongo.

Mimi naanza na hawa; Mark Sirengo, Haruna Niyonzima, Mike Katende.
 
Mbuyu twite huyu jamaa yuko poa sana

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Aliyemuona constantine kimanda bila shaka atakubaliana na mimi kuwa hakujatokea beki bora kama yule kwa miaka ile mpaka sasaivi

Nakumbuka mechi ya simba na yangu nimesahau mwaka, labda 92/93. Constantine Kimanda fullback Five na George Masatu simba Fullback wa msimbazi. Simba ilianza kuwafunga yanga kwa mpira wa adhabu ndogo, goli aligunda Masatu, likasawazishwa na Kimanda kwa style ile ile ya Masatu adhabu ndogo. Kilichonifurahisha na kinachonifanya nimkumbuke huyu bwana na jinsi alivyopiga ile faulo. Mwameja aliruka kuokoa mpira lakini alikosea kutaim spidi ya mpira, wakati anarudi chini baada ya kuruka mpira ndo unampita kwenda wavuni.
Bottom line, Kimanda alikuwa mchezaji mzuri sana na kama ingekuwa leo angecheza England, au nchi yoyote Ulaya
 
Inasikitisha sana kuona jamaa aliishia kucheza uarabuni tu wakati kiwango chake ni mara tatu ya nonda shaban
 
Tumeshuhudia utitiri mkubwa wa wachezaji wa kigeni wakija hapa kwetu kucheza ligi yetu. Wengi wao huwa ni magarasa lakini wachache huwa ni wachezaji haswa.

Ni wachezaji gani wa kigeni uliwahi kuwakubali hasa baada ya kutamba katika ligi yetu ya Bongo.

Mimi naanza na hawa; Mark Sirengo, Haruna Niyonzima, Mike Katende.

Mackenzie Ramadhan, William Fanbuleh (sina uhakika kama jina lake la pili ndivyo linavyoandikwa), Ngandou Ramadhan.
 
Mmemsahau, William fanbula Double striker na George Opong Weah timu ya taifa ya Liberia.
 
Ramadhani Waso, Mark Sirengo, Emmanuel Okwi, Patrick Mutesa Mafisango, Felix Sunzu, Hamis Kiiza, Amis Tambwe, Haruna Niyonzima, Mbuyu Twite, Kipre Tchetche, Yaw Berko, Pascal Wawa.
Huyo Jamaa Mark Sirengo alikuwa hatari sana, ila mchezaji wa kigeni ambae alikuwa natamani siku zote awe anapata Majeraha ni Emmanuel Okwi, jamaa huyu alikuwa hatari kwa timu pinzani.
Siku ya game ya Yanga na Simba huyu ndie mchezaji niliyekuwa namuogopa.
 
Back
Top Bottom