Wachezaji wa Mamelodi Sundowns wamewaomba mashabiki wao ambao ni Watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya mechi yao dhidi ya Yanga

Wachezaji wa Mamelodi Sundowns wamewaomba mashabiki wao ambao ni Watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya mechi yao dhidi ya Yanga

Wachezaji wa Mamelodi Sundowns Denis Onyango ,Khuliso Mudau na Rivaldo Coetzee wamewaomba mashabiki wao ambao ni watanzania kujitokeza kwa wingi siku ya mechi yao dhidi ya Yanga ili kuwapa motisha kwenye mchezo huo

Mudau
“Tunawaomba Mashabiki wetu wa Tanzania waje kutupa sapoti dhidi ya Yanga ,sapoti yenu itatupa nguvu ya kupambana asante”

Rivaldo
“Mashabiki wa Mamelodi ambao mpo Tanzania tunaomba mjitokeze kutupa sapoti tutakapocheza na Yanga hapo Tanzania “

Onyango
“Mambo vipi watanzania ,tunashauku kubwa ya kukutana na mashabiki wetu tutakapocheza na Yanga kwenye mechi ya CAF champions league dhidi ya Yanga , tunaona comments na tweets zenu tukutane Tanzania”

Haya kolozdad GENTAMYCINE , OKW BOBAN SUNZU, Kalpana nendeni mkawashuhudie wazulu wenzenu wakipigwa kipigo Cha mbwa Koko na Yanga Sc.
Ndumbaro katupiga Pini ili kuwalinda Utopolo.
 
Unajua hii kitu itapaisha sana upinzani wa Yanga na Simba huko Africa tukiiendekeza. Yaani tutajulikana sana. Sijajua kama italeta matokeo + au - ila ninachojua tutajulikana.
Kwani Orlando Pirates na Kaizer Chiefs walishamaliza upinzani wao mana tuliujua hadi huku Tanzania?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom