Wachezaji wa SBS walipewa uraia kimagumashi, kuna matumizi mabaya ya madaraka

Wachezaji wa SBS walipewa uraia kimagumashi, kuna matumizi mabaya ya madaraka

Kibu denga alipewaje uraia. Kwa vigezo gani vilitumika?

Nashauri tusipende double standards
Wengi mmeanza kumjua Kibu Denis alipohamia Simba.

Una taarifa huyu Kibu Denis hadi kambi ya wakimbizi ameishi na amecheza sana ndondo kwenye timu za Kigoma pale?
 
Wewe jamaa ni liongo sana Kibu yupo Tanzania toka 1998 wakitokea Congo. Geita na Mbeya City kwenye kacheza miaka 5. Kuhusu wapi kazaliwa mimi sijui na sijasema kazaliwa Congo
Kibu ana miaka 26
1998 mpaka Sasa ni miaka 27
Kwaiyo ina maana Kibu alikuwa nchini kabla ya kuzaliwa😅
 
Wengi mmeanza kumjua Kibu Denis alipohamia Simba.

Una taarifa huyu Kibu Denis hadi kambi ya wakimbizi ameishi na amecheza sana ndondo kwenye timu za Kigoma pale?
Ndugu usiongee vitu ikiwa humjui unayemwambia. Jikite kwenye hoja usiongee vingine utafedheheshwa
 
Kibu denga alipewaje uraia. Kwa vigezo gani vilitumika?

Nashauri tusipende double standards
Kibu alizaliwa Kigoma kwenye kambi ya ukimbizi na wakati anapewa uraia alikuwa ameshaishi Tanzania zaidi ya miaka 10; mpaka leo mama yake bado anaishi Kigoma. Siyo hawa wakuja mwaka jana tu na kupewa uraia leo.
 
Kipande cha Sheria ya Uraia

Second Schedule (Section 9(1))
Conditions for citizenship by naturalisation
1. Subject to the provisions of the next following paragraph, the qualifications for naturalisation of an alien
who applies for it are—
(a) that he has resided in the United Republic throughout the period of twelve months immediately
preceding the date of the application; and
(b) that during the ten years immediately preceding the said period of twelve months he resided in the
United Republic for periods amounting in the aggregate to not less than seven years; and
(c) that he has an adequate knowledge of Kiswahili or the English language; and
(d) that he is of good character; and
(e) that, in terms of his past and potential contribution to the national economy, scientific and
technological advancement and to the national social and cultural welfare, he would be a suitable
citizen of the United Republic;
(f) that he intends, if naturalised, to continue to reside permanently in the United Republic.
2. If in the special circumstances of any particular case the Minister thinks fit, he may—
(a) allow a continuous period of twelve months ending not more than six months before the date of
application to be reckoned for the purposes of subparagraph (a) of paragraph 1 as though it had
immediately preceded that date;
(b) allow periods of residence earlier than eight years before the date of application to be reckoned in
computing the aggregate mentioned in subparagraph (b) of paragraph 1.

Ufafanuzi wangu​

Mgeni anayetaka kuomba Uraia wa Tanzania anapaswa kuwa na sifa zifuatazo​

i. Mwombaji awe na umri wa miaka 18 au zaidi na awe na uwezo wa kufanya maamuzi yanayokubalika kwa mujibu wa sheria za nchi​

ii. Awe ameishi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muda wa miezi 12 mfululizo kabla ya kutuma maombi​

iii. Katika muda wa miaka kumi kabla ya miezi kumi na mbili hiyo awe ameishi ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muda usiopungua miaka saba​

iv. Awe anaelewa vizuri lugha ya Kiswahili au Kiingereza​

v. Awe na tabia njema/nzuri​

vi. Awe alichangia na ataendelea kuchangia katika ukuzaji wa uchumi, Sayansi na Teknolojia na utamaduni wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania​

vii. Awe anakusudia kuishi moja kwa moja ndani ya Jamhuri ya Muungano ikiwa ombi lake la uraia litakubaliwa​


My Take
Kwa vigezo hivyo wachezaji wa SBS waliopewa uraia hawakidhi vigezo hivyo. Bila kuweka ushabiki ni dhahiri hili jambo limefanyika kisiasa. Niliwasikiliza wachambuzi wa michezo kipindi cha AM Azam HD1 walionyesha mashaka juu ya namna wachezaji wa SBS walivyopewa uraia. Nami nanusa matumizi mabaya ya madaraka ya kiongozi wa SBS. Ni busara Rais amuweke pembeni anayetajwa, uchunguzi ufanyike na achukuliwe hatua za kisheria.
Tusiende mbali, Kibu alitimiza vigezo?
 
Wewe jamaa ni liongo sana Kibu yupo Tanzania toka 1998 wakitokea Congo. Geita na Mbeya City kwenye kacheza miaka 5. Kuhusu wapi kazaliwa mimi sijui na sijasema kazaliwa Congo
Hata kwa kigezo hiki anakosa sifa, maana alikuwa anaishi kinyume cha sheria.
 
Yote kwa yote kilichonifurahisha hapa ni hiyo kauli ya Madeleka full stop. Mbivu na mbichi zijulikane wazi mahakamani basi. Na hao SBS waendelee kufanya mzaha na hili suala lakini wakumbuke kuwa hili suala likiwa la moto hao TFF na serikali watawatema na timu itashuka daraja kiutani utani.

Simba na Yanga nazo zikifungwa na hao jamaa nazo mashabiki na viongozi wao wakikaza kuna poiniti za bure kabisa bila mjadala.
 
Sio kweli Kibu alikuja bongo akiwa mtu mzima
Na wala Kibu hakuwahi kuwa mkimbizi
Kuna kipindi alihojiwa akiwa Mbeya city hata kiswahili kilimshinda
Uovu upingwe wazi hata kama ulifanywa na Simba
Acha uongo
 
Back
Top Bottom