Wachezaji wa SBS walipewa uraia kimagumashi, kuna matumizi mabaya ya madaraka

Kibu denga alipewaje uraia. Kwa vigezo gani vilitumika?

Nashauri tusipende double standards
Wengi mmeanza kumjua Kibu Denis alipohamia Simba.

Una taarifa huyu Kibu Denis hadi kambi ya wakimbizi ameishi na amecheza sana ndondo kwenye timu za Kigoma pale?
 
Wewe jamaa ni liongo sana Kibu yupo Tanzania toka 1998 wakitokea Congo. Geita na Mbeya City kwenye kacheza miaka 5. Kuhusu wapi kazaliwa mimi sijui na sijasema kazaliwa Congo
Kibu ana miaka 26
1998 mpaka Sasa ni miaka 27
Kwaiyo ina maana Kibu alikuwa nchini kabla ya kuzaliwa😅
 
Wengi mmeanza kumjua Kibu Denis alipohamia Simba.

Una taarifa huyu Kibu Denis hadi kambi ya wakimbizi ameishi na amecheza sana ndondo kwenye timu za Kigoma pale?
Acha uongo
 
Wengi mmeanza kumjua Kibu Denis alipohamia Simba.

Una taarifa huyu Kibu Denis hadi kambi ya wakimbizi ameishi na amecheza sana ndondo kwenye timu za Kigoma pale?
Ndugu usiongee vitu ikiwa humjui unayemwambia. Jikite kwenye hoja usiongee vingine utafedheheshwa
 
Kibu denga alipewaje uraia. Kwa vigezo gani vilitumika?

Nashauri tusipende double standards
Kibu alizaliwa Kigoma kwenye kambi ya ukimbizi na wakati anapewa uraia alikuwa ameshaishi Tanzania zaidi ya miaka 10; mpaka leo mama yake bado anaishi Kigoma. Siyo hawa wakuja mwaka jana tu na kupewa uraia leo.
 
Tusiende mbali, Kibu alitimiza vigezo?
 
Wewe jamaa ni liongo sana Kibu yupo Tanzania toka 1998 wakitokea Congo. Geita na Mbeya City kwenye kacheza miaka 5. Kuhusu wapi kazaliwa mimi sijui na sijasema kazaliwa Congo
Hata kwa kigezo hiki anakosa sifa, maana alikuwa anaishi kinyume cha sheria.
 
Yote kwa yote kilichonifurahisha hapa ni hiyo kauli ya Madeleka full stop. Mbivu na mbichi zijulikane wazi mahakamani basi. Na hao SBS waendelee kufanya mzaha na hili suala lakini wakumbuke kuwa hili suala likiwa la moto hao TFF na serikali watawatema na timu itashuka daraja kiutani utani.

Simba na Yanga nazo zikifungwa na hao jamaa nazo mashabiki na viongozi wao wakikaza kuna poiniti za bure kabisa bila mjadala.
 
Sio kweli Kibu alikuja bongo akiwa mtu mzima
Na wala Kibu hakuwahi kuwa mkimbizi
Kuna kipindi alihojiwa akiwa Mbeya city hata kiswahili kilimshinda
Uovu upingwe wazi hata kama ulifanywa na Simba
Acha uongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…