Wachezaji wa Simba wafanyiwa vipimo vya Afya katika Hospitali ya Mloganzila

Wachezaji wa Simba wafanyiwa vipimo vya Afya katika Hospitali ya Mloganzila

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Simba wamefika Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa afya zao na kufanya vipimo mbalimbali ikiwa ni maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya ya mashindano ya ligi 2023/2024.
Duchu.jpg

Daktari wa Timu ya Simba Dkt. Edwin Kagabo amesema kuwa lengo la kuja kufanya uchunguzi Muhimbili Mloganzila ni kujua hali ya wachezaji wao kiafya kabla hawajaanza kupatiwa mazoezi ya msimu mpya.
Kennedy.jpg

“Kwetu sisi kama idara ya tiba na afya msimu wetu ndio umeanza, tumekuja katika hospitali hii kufanya uchunguzi wa afya ambapo tutafanya vipimo mbalimbali na tutajikita zaidi katika kuangalia mafuta mwilini pamoja na uzito kwasababu hivi vyote kwa namna moja au nyingine vinaweza kuathiri performance ya wachezaji wetu hivyo ni muhimu tujiridhishe kabla ya kuanza msimu huo” Amesema Dkt.Kagabo.
Phiri.jpg

Vipimo vilivyofanyanyika ni X-Ray ya kifua uchunguzi wa damu, utendaji kazi wa moyo kwa kufanya kipimo cha ECG, ECO pamoja na kipimo cha Ultrasound.
 
MPIRA wetu una madudu mengi mno.
Tukiandika hapa HATUWEZI kumaliza.


1. Simba Ina TATIZO KUBWA sana kwenye No 6.
Hadi saizi nafasi zimejaa hakuna waliemsajili UJINGA mtupu

Hadi sasa Wamesajili JUMLA ya mawinga 11.

2. Eneo la beki wa kati
MSIMU uliopita lilikuwa na Inonga, onyango, Ottara Nyoni na KENEDY JUMA.
Eo hii wamebakiwa na wachezaji watatu tu3 Mabeki, hata wakijigawa mazoezini hawatoshi.

UONGOZI WA SIMBA AMKENI ACHENI UPUMBAVU
 
Back
Top Bottom