Wachezaji wa Yanga SC wagomea mazoezi

Wachezaji wa Yanga SC wagomea mazoezi

gambe96

Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
5
Reaction score
2
Wachezaji wa Yanga wamegomea mazoezi ya leo Ijumaa, huku benchi la Ufundi wakibaki na mshangao kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MCL Digital, Meneja wa Yanga, Salehe Hafidhi amethibitisha kwamba wachezaji watatu wageni ndio waliojitokeza kwenye mazoezi ya leo asubuhi.

Wachezaji hao ni Deus Kaseke, Mrisho Ngassa na Heritier Makambo ambao wote hao wamesajili kweye dirisha la msimu huu.

Hafidhi alisema sababu kubwa ambazo amezipata juu ya wachezaji hao kugoma ni kutokana na madai yao ya fedha.

Aliongeza kuwa ameshawasilina na uongozi ili kujua nini cha kufanya isipokuwa benchi la ufundi litaendelea na ratiba yake ya mazoezi kama kawaida kesho Jumamosi Asubuhi.

Timu hiyo inapita katika kipindi kigumu kutokana na kuwepo na taarifa kwamba inakabiliwa na ukata.

Jumatano wiki hii kikosi cha Yanga kiliambulia kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Gor Mahia katika mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Afrika.
 
Hadi hela ya mishahara nayo ni shida? Ile kamati ilisema hakuna mchezaji anayedai mshahara sasa nani anasema ukweli?

Mimi naipenda Yanga ila msimu ujao tunakwenda daraja la 1 kirahisi kabisa
 
Wapi Mzee Akilimali a.k.a Abromovic.. sasa ndio muda wa kuiteka timu kirahisi usisubiri watu waendeshe ulete chokochoko!
 
Uchawi ni pale Fei Toto anapoikacha Singida Utd na kujiunga na wachezaji wanaushinda na kulala njaa
 
Wachezaji wa Yanga wamegomea mazoezi ya leo Ijumaa, huku benchi la Ufundi wakibaki na mshangao kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MCL Digital, Meneja wa Yanga, Salehe Hafidhi amethibitisha kwamba wachezaji watatu wageni ndio waliojitokeza kwenye mazoezi ya leo asubuhi.

Wachezaji hao ni Deus Kaseke, Mrisho Ngassa na Heritier Makambo ambao wote hao wamesajili kweye dirisha la msimu huu.

Hafidhi alisema sababu kubwa ambazo amezipata juu ya wachezaji hao kugoma ni kutokana na madai yao ya fedha.

Aliongeza kuwa ameshawasilina na uongozi ili kujua nini cha kufanya isipokuwa benchi la ufundi litaendelea na ratiba yake ya mazoezi kama kawaida kesho Jumamosi Asubuhi.

Timu hiyo inapita katika kipindi kigumu kutokana na kuwepo na taarifa kwamba inakabiliwa na ukata.

Jumatano wiki hii kikosi cha Yanga kiliambulia kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Gor Mahia katika mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Ni utahira sijui wa kiwango gani kuwa kiongozi wa team kubwa kama Yanga, yenye mashabiki kila pembe ya nchi hii, wenye uhitaji wa kila bidhaa yenye nembo ya club yao kuanzia kikombe, maji, tshirt, shoes, ndala, watches, belt,shuka, mataulo, etc kukosa pesa za kuongoza club kubwa kama Yanga, sina hakika kama hao viongozi wana hata theduthi ya akili kwenye bongo zao...
 
Ni wakati sasa wa Mzee Akilimali kukabidhiwa timu kama alivyokuwa anaitaji!!
 
Yaani mizengwe na fujo zote zilizotokea Yanga hapa, ni movie inayochezwa na baadhi ya viongozi na wanachama wa Yanga.. Zinalengwa milioni 600 kutoka CAF.. Tuendelee kusubiri lakini its sad, kwamba hii ndo hali halisi ya mpira hapa Tanzania.. Kufika walikofika wenzetu ni ndoto..
 
WACHEZAJI wote wa Yanga unaowajua wewe ambao usajili wao upo CAF jana Ijumaa waligoma kufanya mazoezi huku Kocha Mwinyi Zahera akiwasihi viongozi wawaambie mashabiki wa timu hiyo ukweli.

Zahera alifika mazoezini kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini asubuhi akajikuta yupo na wachezaji watano tena wote ni wageni wengine hata mashabiki wa Yanga hawawajui.

Wachezaji wote waliocheza mechi ya Gor Mahia hakuna hata mmoja aliyeonekana mazoezini na Zahera hakuwa na taarifa yoyote lakini Championi limejiridhisha kwamba wameambizana kugoma kufanya mazoezi wakishinikiza walipwe mishahara yao ya miezi mitatu na kushinikiza pia mashabiki wajitokeze kuokoa jahazi.

Yanga Jumatano ya wiki hii ilipigwa mabao 4-0 na Gormahia kwenye mechi ya Shirikisho na timu hizo zitarudiana Dar es Salaam Ijumaa ijayo saa 1.00 usiku.

Zahera ambaye si mzungumzaji sana jana Ijumaa aliamua kufunguka mpaka tone la mwisho kwa viongozi akiwambia wawaambie mashabiki na wanachama ukweli kuinusuru timu hiyo na kumrahisishia kazi yake.

Zahera alipofika uwanjani hapo alikuta kuna wachezaji watano pekee ambao ni; Deus

Kaseke, Heritier Makambo, Mrisho Ngasa, Emeka Emerun na Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ hali iliyomfanya asitishe mazoezi hayo mpaka leo Jumamosi.

“Kiukweli uongozi wangu unanipa wakati mgumu sana wa kuifundisha hii timu, kwani ni vigumu sana kwa sasa kutegemea kupata matokeo kwenye mchezo ujao wa marudiano dhidi ya Gor Mahia kwa staili hii ya wachezaji kuwa na kasumba ya kukimbia mazoezi kila kukicha.

“Naomba viongozi wangu waache kuficha ukweli badala yake wajitokeze hadharani wawaambie mashabiki kuwa timu inamatatizo ya kifedha ili kama kuna ambaye ataguswa na kuona kuna haja ya kuichangia afanye hivyo ili wanipunguzie mzigo wa kugombana na wachezaji kama leo ambapo tulielewana tuanze mazoezi lakini wote waliokuwa safarini hawajatokea,”alisema Kocha huyo raia wa Ufaransa.

“Nimeshindwa kufanya mazoezi leo kutokana na kukutana na wachezaji watano tu na hawa wote hakuna hata mmoja ambaye naweza kumtumia kwenye mechi ijayo kutokana na wote hao hakuna aliye na leseni ya Caf.

“Kama watagoma zaidi ya siku tatu zijazo maana yake ni kwamba hata uwezekano wa kucheza mechi ijayo utakuwa mgumu kwetu lakini hata hivyo kupata matokeo pia itakuwa ni hadithi tu,” alisema Zahera ambaye msaidizi wake aliyetua hivi karibuni ameshaingia mitini.

Alipotafutwa Kaimu Mwenyeki wa Yanga, Clement Sanga alisema: “Kwa sasa nipo nje ya ofisi siwezi kuzungumza lolote mpaka nitakaporejea kesho (leo).
 
Nina wazo: Ili kuinua Ligi kuu iwe na mapato serikali inaweza kulazimisha Vingamuzi na kuweka Program ya kuonyesha mechi za Ligi kuu, Ligi Daraja la kwanza na Ligi Daraja la pili. Ikawepo collecting system ya kucollect Elfu tano kwa kila king'amuzi kwa kila mwezi ambazo zitakuwa directed kwenda kwa vilabu. Nikiassume kuwa kuna ving'amuzi 20,000,000 nchini basi Inaweza kukusanywa trilioni 1.2 kwa kila mwaka ambazo zitakuwa distributed kwa timu hizo. Kuliko hivi sasa Kina Mo Dewji na Manji kutegemewa kutoa hela zao za mifukoni kuviendesha vilabu
 
Nina wazo: Ili kuinua Ligi kuu iwe na mapato serikali inaweza kulazimisha Vingamuzi na kuweka Program ya kuonyesha mechi za Ligi kuu, Ligi Daraja la kwanza na Ligi Daraja la pili. Ikawepo collecting system ya kucollect Elfu tano kwa kila king'amuzi kwa kila mwezi ambazo zitakuwa directed kwenda kwa vilabu. Nikiassume kuwa kuna ving'amuzi 20,000,000 nchini basi Inaweza kukusanywa trilioni 1.2 ambazo zitakuwa distributed kwa timu hizo. Kuliko hivi sasa Kina Mo Dewji na Manji kutegemewa kutoa hela zao za mifukoni kuviendesha vilabu vyetu vikubwa!
China yenye watu takribani bilioni kadhaa haina hivyo ving'amuzi 20,000,000.

Tanzania ina watu takribani milioni 50 hizo ndoto zako za kuwa na ving'amuzi million 20 labda baada ya miaka elfu 10 ijayo.
 
China yenye watu takribani bilioni kadhaa haina hivyo ving'amuzi 20,000,000.

Tanzania ina watu takribani milioni 50 hizo ndoto zako za kuwa na ving'amuzi million 20 labda baada ya miaka elfu 10 ijayo.
Exactly
 
China yenye watu takribani bilioni kadhaa haina hivyo ving'amuzi 20,000,000.

Tanzania ina watu takribani milioni 50 hizo ndoto zako za kuwa na ving'amuzi million 20 labda baada ya miaka elfu 10 ijayo.
Anafananisha bei ya King'amuzi na bei ya SIM CARD
 
Huyu clement sanga ndo tatizo

Tatizo siyo Clement Sanga peke yake...tatizo ni wanaYanga wote....ni mambo ya kupenda vya dezo...alipokuwepo Manji walidhani kuwa sasa Yanga imefika...hawakujua kuwa Yanga na mipsa yake ndiye aliyeifanya Yanga iwe kama ilivyo sasa...mishahara ya wachezaji imekuwa inflated...gharama za usajili wa wachezaji zimekuwa inflated...mchezaji anasajiliwa kwa milioni 200 kumbe mchezaji anapokea sh. milioni 50 tu nyingine zinaingia mikononi mwa wapigaji, madalai, makomandoo, wapiga domo na majungu na kadhalika....Kocha wa timu anakuwa Katibu Mkuu, wapi na wapi...Katibu Mkuu ni mtendaji na ni lazima awe mwenye taaluma ya menejimenti...Katibu Mkuu hata kuzungumza na media hajui, anazungumza utafikiri anazungumza na washikaji wa kijiweni...viongozi hawajui matatizo ya wachezaji, hawajui wachezaji wamelalaje, wanadhani suluhisho ni pesa..tatizo la Yanga ni zaidi ya pesa..hakuna weledi katika uongozi...viongozi wamekusanywa tu hawana hili wala lile...mchezaji anasajiliwa mtu anaibuka kwenye vyombo vya habari na kusema'nimesajili' huyu na yule badala ya kusema Yanga imesajili...mtu anataka apate sifa yeye na siyo klabu..dah...ngoja Yanga waipate...Mwenyekiti wa matawi ana nguvu kuliko viongozi wa timu...yaani wale waliokuwa kwenye Yanga asili na Yanga kampuni wanarudi na migogoro ya nyuma...
 
Back
Top Bottom