Wachezaji wa Yanga SC wagomea mazoezi

Wachezaji wa Yanga SC wagomea mazoezi

WACHEZAJI wote wa Yanga unaowajua wewe ambao usajili wao upo CAF jana Ijumaa waligoma kufanya mazoezi huku Kocha Mwinyi Zahera akiwasihi viongozi wawaambie mashabiki wa timu hiyo ukweli.

Zahera alifika mazoezini kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini asubuhi akajikuta yupo na wachezaji watano tena wote ni wageni wengine hata mashabiki wa Yanga hawawajui.

Wachezaji wote waliocheza mechi ya Gor Mahia hakuna hata mmoja aliyeonekana mazoezini na Zahera hakuwa na taarifa yoyote lakini Championi limejiridhisha kwamba wameambizana kugoma kufanya mazoezi wakishinikiza walipwe mishahara yao ya miezi mitatu na kushinikiza pia mashabiki wajitokeze kuokoa jahazi.

Yanga Jumatano ya wiki hii ilipigwa mabao 4-0 na Gormahia kwenye mechi ya Shirikisho na timu hizo zitarudiana Dar es Salaam Ijumaa ijayo saa 1.00 usiku.

Zahera ambaye si mzungumzaji sana jana Ijumaa aliamua kufunguka mpaka tone la mwisho kwa viongozi akiwambia wawaambie mashabiki na wanachama ukweli kuinusuru timu hiyo na kumrahisishia kazi yake.

Zahera alipofika uwanjani hapo alikuta kuna wachezaji watano pekee ambao ni; Deus

Kaseke, Heritier Makambo, Mrisho Ngasa, Emeka Emerun na Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ hali iliyomfanya asitishe mazoezi hayo mpaka leo Jumamosi.

“Kiukweli uongozi wangu unanipa wakati mgumu sana wa kuifundisha hii timu, kwani ni vigumu sana kwa sasa kutegemea kupata matokeo kwenye mchezo ujao wa marudiano dhidi ya Gor Mahia kwa staili hii ya wachezaji kuwa na kasumba ya kukimbia mazoezi kila kukicha.

“Naomba viongozi wangu waache kuficha ukweli badala yake wajitokeze hadharani wawaambie mashabiki kuwa timu inamatatizo ya kifedha ili kama kuna ambaye ataguswa na kuona kuna haja ya kuichangia afanye hivyo ili wanipunguzie mzigo wa kugombana na wachezaji kama leo ambapo tulielewana tuanze mazoezi lakini wote waliokuwa safarini hawajatokea,”alisema Kocha huyo raia wa Ufaransa.

“Nimeshindwa kufanya mazoezi leo kutokana na kukutana na wachezaji watano tu na hawa wote hakuna hata mmoja ambaye naweza kumtumia kwenye mechi ijayo kutokana na wote hao hakuna aliye na leseni ya Caf.

“Kama watagoma zaidi ya siku tatu zijazo maana yake ni kwamba hata uwezekano wa kucheza mechi ijayo utakuwa mgumu kwetu lakini hata hivyo kupata matokeo pia itakuwa ni hadithi tu,” alisema Zahera ambaye msaidizi wake aliyetua hivi karibuni ameshaingia mitini.

Alipotafutwa Kaimu Mwenyeki wa Yanga, Clement Sanga alisema: “Kwa sasa nipo nje ya ofisi siwezi kuzungumza lolote mpaka nitakaporejea kesho (leo).
mzee wenu Akilimali yu wapi?

si alisema klabu haimuhitaji Manji wamwachie yeye (Akilimali) aongoze??

mkabidhini timu huyo mzee afanye yake bana!!
 
Zahera alifika mazoezini kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini asubuhi akajikuta yupo na wachezaji watano tena wote ni wageni wengine hata mashabiki wa Yanga hawawajui.
Kaseke, Heritier Makambo, Mrisho Ngasa, Emeka Emerun na Feisal Salum Abdallah ‘Fei Toto’ hali iliyomfanya asitishe mazoezi hayo mpaka leo Jumamosi.
Mrisho amekana lini, uraia wa Tanzania? Uandishi huu unaudhi!!
 
Wachezaji wa Yanga wamegomea mazoezi ya leo Ijumaa, huku benchi la Ufundi wakibaki na mshangao kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MCL Digital, Meneja wa Yanga, Salehe Hafidhi amethibitisha kwamba wachezaji watatu wageni ndio waliojitokeza kwenye mazoezi ya leo asubuhi.

Wachezaji hao ni Deus Kaseke, Mrisho Ngassa na Heritier Makambo ambao wote hao wamesajili kweye dirisha la msimu huu.

Hafidhi alisema sababu kubwa ambazo amezipata juu ya wachezaji hao kugoma ni kutokana na madai yao ya fedha.

Aliongeza kuwa ameshawasilina na uongozi ili kujua nini cha kufanya isipokuwa benchi la ufundi litaendelea na ratiba yake ya mazoezi kama kawaida kesho Jumamosi Asubuhi.

Timu hiyo inapita katika kipindi kigumu kutokana na kuwepo na taarifa kwamba inakabiliwa na ukata.

Jumatano wiki hii kikosi cha Yanga kiliambulia kipigo cha mabao 4-0 kutoka kwa Gor Mahia katika mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Wagome tu hakuna namna.
 
Tatizo siyo Clement Sanga peke yake...tatizo ni wanaYanga wote....ni mambo ya kupenda vya dezo...alipokuwepo Manji walidhani kuwa sasa Yanga imefika...hawakujua kuwa Yanga na mipsa yake ndiye aliyeifanya Yanga iwe kama ilivyo sasa...mishahara ya wachezaji imekuwa inflated...gharama za usajili wa wachezaji zimekuwa inflated...mchezaji anasajiliwa kwa milioni 200 kumbe mchezaji anapokea sh. milioni 50 tu nyingine zinaingia mikononi mwa wapigaji, madalai, makomandoo, wapiga domo na majungu na kadhalika....Kocha wa timu anakuwa Katibu Mkuu, wapi na wapi...Katibu Mkuu ni mtendaji na ni lazima awe mwenye taaluma ya menejimenti...Katibu Mkuu hata kuzungumza na media hajui, anazungumza utafikiri anazungumza na washikaji wa kijiweni...viongozi hawajui matatizo ya wachezaji, hawajui wachezaji wamelalaje, wanadhani suluhisho ni pesa..tatizo la Yanga ni zaidi ya pesa..hakuna weledi katika uongozi...viongozi wamekusanywa tu hawana hili wala lile...mchezaji anasajiliwa mtu anaibuka kwenye vyombo vya habari na kusema'nimesajili' huyu na yule badala ya kusema Yanga imesajili...mtu anataka apate sifa yeye na siyo klabu..dah...ngoja Yanga waipate...Mwenyekiti wa matawi ana nguvu kuliko viongozi wa timu...yaani wale waliokuwa kwenye Yanga asili na Yanga kampuni wanarudi na migogoro ya nyuma...
Uko sahihi kabisa mkuu,salute
 
Hawa yanga shida wameshindwa kuishi kwa bajeti,
Sasa unawachezaji uliowasajili hujawalipa afu unaenda kusajili wachezaji wengine kuongeza gharama tu.
Kwa nini wasiwalipe kwanza wachezaji walionao ili wawe na morali ya kuipigania badge ya yanga badala ya kuongeza gharama za kuwasajili akina ngasa.
Hiyo timu iliyokuwepo ilikua inafanya vizr tu kipindi mishahara yao na posho wanapewa.
Yanga msifanye usajili ili muonekane ishi kwa bajeti yenu ili wachezaji wawe na morali.
 
Aiseee yanga jina kubwa ila sasa walafi wamelipunguzia hadhi vibaya mno
 
Mrisho amekana lini, uraia wa Tanzania? Uhandishi huu unaudhi!!
andika, uandishi; ila ktk kiswahili hatuna maneno 'handika', 'uhandishi';
halafu katumia 'wageni' huenda akimaanisha wapya, waliosajiliwa, wageni ktk club
 
Kuna wale wazee huwa wanachonga Sana, wajitokeze kutoka mafichoni walikombie chama.
 
Yajayo yanafurahisha. Daraja lazma washuke msimu huu. Bundi kashatua na kagoma ondoka.
 
Huyu clement sanga ndo tatizo
Sidhani kama Sanga ndo Tatizo,
Wana Yanga mnamlaumu Sanga kwa sababu mlishazoea akiwa mwenyekiti anatoa hela mfukoni kuisapoti timu.
Yanga mlitakiwa kumlaumu Manji ambae aliwafanya mtegemee yeye hata mlikua hamfikirii ka kunakuchanga ada ya uanachama.
Tengenezeni mfumo mzr sio kumlaumu Sanga.
Labda kama wanachama mmeshachangia team sasa kala
 
Back
Top Bottom