Wachezaji wa zamani wa Yanga mtaakaoenda kumpongeza Zahera msisahau kuliongelea la Kakolanya

Wachezaji wa zamani wa Yanga mtaakaoenda kumpongeza Zahera msisahau kuliongelea la Kakolanya

Ulimakafu

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Posts
31,248
Reaction score
13,244
Nawapongeza wachezaji wa zamani wa Yanga ambao wanaenda kuongea na kumpongeza kocha mkuu wa timu Yanga kwa kile alichofanya mpaka sasa akiwa katika mazingira magumu. Wasisahau kumdokezea kuhusu suala la kipa Beno Kakolanya. Makipa tuliobakiwa nao akiumia mmoja imekula kwetu. Tukumbuke pia sisi wanadamu tuna mapungufu yetu, mtoto akiunyea mkono dawa si kuukata. Mpaka sasa kama ni kujifunza na kubadilika atakuwa kashafanya hivyo.
Bandugu nawasilisha.
 
Kwa maoni yangu, wasijaribu kabisa.
Unachopaswa kuelewa nia kwamba kuna wachezaji kama 18 hivi ambao wanadai mishahara pamoja na marupurupu kwa kipindi kirefu tu lakini bado wanajitoa kucheza kama vile hawana matatizo. Huyu Kakolanya aligoma na akatokea mshitiri akajitangaza rasmi kuwa amemlipa. Kwa kufanya hivyo huoni kumrejesha huyo golkipa ni kukaribisha mgomo kwa wachezaji wengine?????
Lazima kuwe na msimamo mkali na ni Yanga tu yenye mila ya aina hii kwani kama iliweza kufukuza wachezaji wote wa timu[kutokana na nidhamu] na bado ikaendelea.
Mwinyi Zahera ninamfananisha sana na Tambwe Leya.
'Daima mbele Nyuma mwiko'
 
Amekosekana mfadhili wa kuwalipa hao wachezaji wote wanaodai halafu kakulanya akajiunga na wenzake? Yanga timu kongwe kuliko zote Tanzania . Si amini kinachoendelea. Suluhusho.
Rostam au Mengi awakope kama Manji hataki.
Tff wafanye uzalendo waachie ela ya kiingilio iende yote Yanga kwenye mechi zake walipe wachezaji .
Michango iratibiwe nchi nzima kwa njia ya airtel,mpesa nk
 
Swala la Kakolanya ni complicated asee. Simwamini Kabwili ila Siamini zaidi uamuzi wa kumrudisha Kakolanya. Wachezaji wote wamekubali kufa na kupona kujitoa kwa ajili ya timu isipokuwa huyo mmoja. Kakolanya ataenda kuua morali ya timu iliyopo kwa sasa. Ni rahisi kusaivu na kina Kindoki wakati huu kuliko Beno atayeua kabisa molari ya timu nzima. Siungi mkono hoja.
 
Back
Top Bottom