Wachezaji wafuatao wanatuhujumu: Kapombe, Bocco, Manula

tatamajuva

Member
Joined
Sep 11, 2019
Posts
74
Reaction score
84
Wachezaji tajwa hapo juu Kapombe, Bocco na Manula wamejazwa mahela na GSM, ili wasifanye vizuri kwenye mechi mbalimbali za nbc premier league.

Hawajitumi kabisa, wakifika 18 za mpinzani wanatoa pasi za kugongesha wachezaji na hatimaye mpira unakwama.

Nakuthibitishieni kuwa timu inahujumiwa na wachezaji na siyo ubovu wa kocha.

Nashauri chezesheni kikosi Cha pili na baadhi ya wachezaji wa kigeni Kama Chama, Mugalu, Sakho, Kanoute.

Aidha fanyeni matibabu ya uhakika kwa Lwanga, la sivyo hata mechi na Prison tutafungwa.

Kocha Hana tatizo, tatizo lipo kwa wachezaji.
 
Hii ndio lawama ya leo au siku zote?
 
Inapaswa kukubali tu kwamba ligi ni ngumu kila timu imejiandaa vema.
 
Habari za Simba za kuaminika ni za kutoka kwa GENTAMYCINE tu
 
Ukiachana na hao uliowataja. Mechi ya leo imeshuhudia Mazmiru akikosa nafasi ya wazi, Morrison akikosa nafasi ya wazi, Chama nae akikosa nafasi ya wazi. Vipi unalizungumziaje hili.

Mwisho acheni kutafuta sehemu ya kujifichi, timu yenu karibia wote viwango vimeshuka.
 
Vilaza Kama nyie ni hasara kwa taifa usipoitaja gsm nafikiri siku iyo inakuwa mbaya kwenu, gsm amekuwa mme wenu aleti matumizi nyumbani? Gsm ndo aliwaelekeza msajili wazee, gsm ndo aliwaambia msisajili mshambuliaji wa maana, muwe mnaficha ujinga wenu wapuuzi nyie
 
Haya haya baada ya kuichambua timu yenu ,michango ya uwanja iendelee kama kawaida.Kuna tawi Bukoba la Kashozi wana mikungu yao mitatu ya ndizi, vikapu viwili vya senene wana jiuliza watazifikisha vipi au kama Ahmed Ally yupo humu JF akawafuate wanasimba wa Kashozi pira birian ili achukue mizigo na kuipakiza kwenye Yutong ili aiwasilishe pale Msimbazi.
 
Huyo Mmanulo anafikaje golini na kugongesha wachezaji? Mbumbumbu bana.
 
Baba yao huyo GSM naona.
 
Utoh wapuuzi sana.. mnanzisha uzi halafu mnajibizana wenyewe kwa wenyewe.. kweli vyura msimu wa masika umeanza tutasikia kelele nyingi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…