Wachezaji walio-flop msimu huu

Wachezaji walio-flop msimu huu

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Dirisha la usajili katika Majira ya kiangazi yaliyopita, Man Utd walikuwa wanamtaka kwa udi na uvumba winga wa Borussia Dortmund, Sancho ila kwa bahati mbaya wakashindwa kumnasa!

Miezi takribani minne baadae, Sancho amekuwa na fomu mbaya ndani ya uwanja, baada ya kucheza takribani dk 900 bila hata ya kuwa na goli tofauti na ilivyokuwa msimu uliopita. Kama Man Utd wangemnunua leo hii story zote mbaya zingekuwa kwa Ole Gunnar kuwa kaua kipaji cha Sancho.

Sancho ameflop sana, yupo chini ya uwezo wake, sijui ni ule uhamisho ulimgharimu nje ya uwanja? Hatujui

Taja mchezaji unayeona msimu huu anacheza chini ya kiwango chake, tofauti na msimu uliopita...
 
Back
Top Bottom