Wachezaji walipwe vizuri sambamba na elimu ya kifedha

Wachezaji walipwe vizuri sambamba na elimu ya kifedha

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Nimekutana na hii hoja kuwa baadhi ya Wachezaji Wastaafu wanalalamika kuwa hawakuwa wanalipwa vizuri ndio maana maisha sasa yanawawia magumu.

Bila kujiingiza kwenye sakata hili la Fei Toto na wala sina tatizo na Mtu kupigania haki yake ya kulipwa vizuri na ikiwezekana alipwe vizuri kwa kadri anavyojituma.

Ila ni muhimu kuweka rekodi sawa ili kutokupotosha Watu.

Ingawa pia nimeshangazwa niliposikia kuwa kuna wakati alikuwa anakwama na akawa anaomba alipiwe pango.Si kwamba sioni umuhimu wa yeye kupata hizo stahiki lakini napata wasiwasi kama Mtu anayelipwa 4m+ kama anapata changamoto ya kulipa pango ni kama kuna shida mahali juu ya matumizi sahihi ya anachokipata dhidi ya matumizi yake. Sasa vipi akishatoka kwenye hiyo ajira?

Hivi si ni kwamba Mtu unapaswa kushona nguo kutokana na kitambaa ulicho nacho? ni kama anahitaji pia elimu ya usimamizi wa fedha sambamba na pesa zaidi anazopambania.

Wapo waliolipwa mabilioni kwenye soka za kimataifa huko lakini baada ya kustaafu soka wakakwama, na wapo waliolipwa kiasi cha kawaida tu na wamebaki wako vizuri tu hata baada ya kustaafu soka. Na utashangaa huyo anayelalamika kuwa hakuwa analipwa vizuri wakati anacheza alifanikiwa kutengeneza karibia milioni mia mbili au zaidi.

Hivyo suala la mustakabali wa Mchezaji huanza na yeye mwenyewe.

Mambo ya kifedha hayana tofauti, ima uwe uliwahi kuwa Mchezaji, Msanii au Mfanya biashara, tofauti yaweza kuwa labda ni umaarufu tu. Mtu anaweza kustaafu kazi aliyoitumiakia miaka 40 akapewa milioni 200 ya kiinua mgongo na bado akaangukia pua sembuse Mchezaji au Msanii aliyevuna zaidi ya milioni mia mbili kwa miaka mitatu au minne tu?.

Huenda wewe umejaaliwa kipaji ila suala la kujisimamia kifedha kwako ikawa mtihani, na wala hili si la ajabu...hivyo basi ni vizuri Mtu kutafuta ushauri namna nzuri ya kufanya kabla ya kuchelewa.

Ni mtu mwenyewe kujipanga unataka nini, unataka kucheza kwa muda gani, unataka kufanya nini baada ya kustaafu soka n.k. ila ukitaka kukaa tu na kusubiri mambo yaje kama suprise basi ni dhahiri kuwa yataku suprise.

Wanahitaji kukumbushwa mara kwa mara kuwa miaka minne au mitano ijayo hilo pato halitokuwepo.

Mtu unaweza hata kuwekeza kwenye hisa au mifuko ya mitaji ili kuendelea kupata kipato baada ya soka.

Mustakabali wa Mtu ni Mtu Mwenyewe.
 
Muhimu ni hizi Timu zetu zijitafakari..!

We fikiria Makambo 1st Eleven hayupo, Siku Zote yupo benchi...Afu amzidi Fei Kwa Mshahara..? Kweli.?.
 
Back
Top Bottom