Wachezaji wanaosajiliwa wanapimwa Afya zao?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Hakuna video wala taarifa inayoonyesha kuwa kuwapima utimamu wa mwili na akili vinafanyika kabla wachezaji kupewa mikataba ya kuvichezea vilabu. Hii haiwezi kuwa sawa hata kidogo, kila mchezaji anastahili kupita mchujo wa utimamu wa mwili na akili kwanza kabla ya kusainishwa mkataba.

Kuna wachezaji ambao wana majereha, magonjwa ya moyo na afya mbaya ya akili ambayo yanaweza kuhatarisha afya zao uwanjani au kuusumbua uongozi kutokana na shida ya akili (upunguani).
 
Ungekuwa specific kidogo mkuu. Swali lako lipo general sana. Kama ni nchi za wenzetu taratibu zote hizo hufanyika kwa kiwango cha juu sana kwakuwa pamoja na yote hayo kubwa zaidi club zinachukulia mchezaji kama asset kubwa sana kwao na ndio maana wanawekeza pesa nyingi sana kwake.

Kwa hapa Tanzania sidhani kama wanafanya hivyo.
 
Jambo la msingi sana umeandika,kwa hapa bongo timu makini kama Simba inazingatia sana afya na utimamu wa wachezaji,mfano kwa Mkude kumpima utimamu wake wa akilk,lakini pia Simba walifatilia afya ya Shaban Djuma kwa kina wakagundua kuwa huwa anamajeraha ya mara kwa mara wakaamua kuachana nae.
Simba inajopo makini la wataalam wa afya wanaofatilia na kwa ukaribu kabisa afya za wachezaji.
 
kwenda kumpima mtu akili na utimamu wa mwili kufanywe kabla ya kumsajili ili kupata taarifa zake za awali (baseline statistics), sio kwenda kumpima akili katikati ya mhula kama simba walivyotaka kufanya kwa Mkunde kwasababu tabia ya Mkude ndiyo ileile tangu siku ya kwanza anajiunga na simba. Kusema akapimwe akili baada ya kuitumikia simba kwa misimu zaidi ya mitano ilikuwa kumvunjia heshima na kumdhalilisha tu kijana wa watu. Kusajili mchezaji bila kumpima afya yake kunaweza kuhatarisha (worsening) afya yake zaidi kama utamchezesha bila kumpatia matibabu sahihi kwanza apone au anaweza kuigarimu timu kutokana na kuwa nje mara kwa mara.
 
Sahihi unachosema,mchezaji anaweza patiwa vipimo kabla ya usajili lakini hata katikati ya muhula akiwa keshapimwa awali anaweza kupimwa tena endapo kutaonekana viashiria vya afya ama utimamu wake umeathirika,hizi mambo za kupima wachezaji timu bora ya Simba wanafanyaga sana tu,tena kawaida kabisa kwa Simba.
 
Jambo la msingi sana umeandika,kwa hapa bongo timu makini kama Simba inazingatia sana afya na utimamu wa wachezaji,mfano kwa Mkude kumpima utimamu wake wa akilk,lakini pia Simba walifatilia afya ya Shaban Djuma kwa kina wakagundua kuwa huwa anamajeraha ya mara kwa mara wakaamua kuachana nae.
Simba inajopo makini la wataalam wa afya wanaofatilia na kwa ukaribu kabisa afya za wachezaji.
Viongozi wenyewe wa Simba ni wa kupima akili, wanataka Mkude akapimwe akili wakati akiwa hana tatizo huko wako kimya dhidi ya mchezaji anatembea na vichupi uwanjani utadhani yupo Copa Cabana.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Sahihi unachosema,mchezaji anaweza patiwa vipimo kabla ya usajili lakini hata katikati ya muhula akiwa keshapimwa awali anaweza kupimwa tena endapo kutaonekana viashiria vya afya ama utimamu wake umeathirika,hizi mambo za kupima wachezaji timu bora ya Simba wanafanyaga sana tu,tena kawaida kabisa kwa Simba.
Hata wewe wewe na viongozi wa simba mnatakiwa mpimwe akili kwa kosa la kuacha kumpima akili morison hadi akifikia kuvua nguo mbele ya mgeni rasmi na watu wa Simba wakamshangalia bila kumchukulia hatua.
 
Back
Top Bottom