Leonel Ateba Mbinda
JF-Expert Member
- Feb 20, 2023
- 644
- 2,695
Aziz Ki aliposajiliwa Yanga alikuwa akifanya mambo ya hovyo kabisa uwanjani hadi wachambuzi wakawa wanaeleza hasara za kiuhasibu kwa kumsajili kiungo huyo hatari kwa sasa hapa nchini, wengi walimdharau na kumponda kuwa hana uwezo na auzwe, Aziz Ki alikuwa anahitaji kuzoea mazingira ya soka na sasa amejipata, mwanaume huyu boli analijua sio masihara.
Joseph Kaniki Golota naye alikuwa hivi hivi enzi zake, alipokuwa akipangwa na marehemu JAmes Siang'a, mashabiki walikuwa wanamzomea na kulaani kila anaposhika mpira, Kaniki alipojipata ilikuwa balaa enzi zile.
Marehemu Christopher Alex naye ilikuwa hivyo hivyo kila alipokuwa akipangwa ilikuwa vichekesho lakini alipozoea mazingira ya kucheza Simba wakati akitokea Reli ya Morogoro alikuwa balaa wakati wa marehemu James Siang'a.
Mifano iko mingi, akina Chirwa nk, Simba imemsajili Steven Mukwala, Joshua Mutale na Jean Charles Ahoua sio kwa kufanya usanii, hawa wachezaji wana uwezo mkubwa wa kucheza soka, Ahoua kule kwao Ivory Coast ni MVP, Ivory Coast ni moja ya nchi zinazoheshimika kwa kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kusakata gozi la ng'ombe, kuwa MVP ligi ya kule sio jambo dogo, Mukwala amekuwa mfungaji bora, Mutale naye ameng'ara kule Zambia, Mutale tumemuona sana kuliko Ahoua na Mukwala.
Hawa wamekuja kwenye mazingira mengine kabisa ingawa ni Professional players, wanahitaji muda kuzoea ligi na mazingira yetu, nawasikia wengine wakisema mbona Awesu kaclik faster, no, awesu ni mchezaji wa ligi ya bongo miaka nenda rudi, yeye hahitaji kuzoea mazingira, yeye anajua majungu na vijiko vya ligi yetu, akina Ahoua wamepewa matarajio makubwa ndani ya timu, ndio maana Ahoua kila akipewa nafasi anataka kufunga yeye, anaona akimpa Mukwala akifunga sijui itakuwaje, wote wana kiu na njaa ya kuiletea mafanikio.
Simba, wanataka wadhihirishe kuwa simba hawakusajiliwa kwa makosa, Ahoua jana alikuwa akitandika mashuti ya mbali sio kwamba alikuwa anafanya makusudi hapana alikuwa anatafuta bao la kwanza ili kujenga confidence, yale mashuti aliyokuwa akiyapeleka alikuwa anajiuliza mbona kule kwao alikuwa akiyafanya na yalikuwa yanakubali lakini hapa yanakataa, nini tatizo?
Hawa ni wachezaji wazuri lakini nna wasiwasi kuna mambo wameambiwa na uongozi na wao wenyewe wakicheki kwenye clip mbalimbali wanaona kazi wanayo, wamepewa mtihani mgumu, waachwe warelax vinginevyo wataharibikiwa, ombi langu kwa mashabiki wawatie moyo hawa wachezaji kwani wanajitafuta kweli kama alivyosema mashine ya kuongea Ahmed Ally, siku wakijipata tutatafutana hapa hapa.
Soma Pia: Ushauri wangu kwa viongozi wa Simba kuhusu wachezaji wetu vinginevyo tumekwisha
Washabiki wawe wavumilivu, watulivu mchezaji mzuri huwezi kumuona kwa mechi nne au tano, wanahitaji sana kucheza ili kuonyesha kuwa wao wanajua na wamekuja kufanya kazi.