Proved
JF-Expert Member
- Sep 10, 2018
- 32,639
- 42,908
Hao Nkana wako wapi 😂😂😂Mbumbumbu mnaanza kutumbuana mapema kabla Nkana hajaja kuwatumbua
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao Nkana wako wapi 😂😂😂Mbumbumbu mnaanza kutumbuana mapema kabla Nkana hajaja kuwatumbua
Bado unao huu mtazamo ?Kwa uwekezaji wa simba inamaana kuwa inahitaji mafanikio ya ndani na ya njee sasa kwa baadhi ya wachezaji tuliyonao ni vigumu kufanikiwa.
Hawa hawatakiwi kuwepo simba
1.tshabalala
2.gyan
3. Mzamiru
Hawa hawatakiwi kuanza kikosi cha kwanza
1.james kotei
2.john boko
3 tshabalala
4 gyani
5 aish manula
6 wawa
Mi sina cheti cha ukocha ila ukiangalia tu hawa wachezaji hawastahili kuanza kikosi cha kwanza cha simba
Mfano manula ameongezeka uzito sana, amezubaa golini, hajitumi, hayupo active lile goli la kwanza alilofungwa inaonesha alikuwa haendi sambamba na mchezo
James kotei
Sio mbunifu katikati mara nyingi anapiga back pass haipandishi timu.madhara ya back pass maana yake unawachosha mabeki na unaruhusu ushambuliwe mda wote
Tshabalala
Huyu bwana mdogo naona soka limemkataa mapema tofauti na kipindi cha nyuma huyu akipata mpira katika mipira kumi, saba lazima ipotee kwa kupigA pasi ndefu isiyo na macho hana ubunifu sio mwepesi kupandisha timu ni mara chache kumuona amevuka mstari wa katikati katika dkk 90 anaweza akaonekana kwenye kumi na nane ya wapinzani mara nne tu
Gyani
Huyu mara zote ninapoenda taifa mashabiki humpigia kelele kwani anaharibu sana hajui kukaba hajui kupiga cross yani hamna kross atapiga isimgonge beki au kross ikipita basi hiyo inaenda nje
Wawa
Kuwaanzisha wawa na erasto kwa wakati mmoja sio sahihi wawa anaweza kucheza ile one against one ila km ikitokea forwad inayopiga one two pale mbele kama jana basi wawa hupotea vibaya erasto atakiwa aanza na yule mganda
Boko na okwi
Amepoteza kujiamini kelele za mashabiki nje huwa zinampanikishA
Kwa jinsi uchezaji wa kagere, boko na okwi ulivyo inatakiwa aanze na washsmbuliaji wawili halafu kiungo kama dilunga anaongeza nguvu pale katikati
Pia kochA awe anasoma mchezo kwa haraka na kubadilisha mbinu ya mchezo sio ametulia tu
Kama tutaendelea na kikosi cha jana simba hatutafanya vizuri kimataifA msimu huu