Wachezaji Weusi wamefanikiwa kuingiza Ushirikina Uingereza?

ibanezafrica

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
7,261
Reaction score
6,553
Sote tunaujua uwezo wa timu zote za UK, hasa miaka hii kidogo ukioondoa Man city na Liverpool. Timu za ligi hii hutolewa hatua za mwanzo kabisa makombe ya ulaya
Sasa msimu huu timu zote nne za Epl zimetinga fainali... Tena zimeshinda kwa matokeo ya kustaajabisha dunia!
Kwanini hili limetokea? Ina maana kiwango cha mpira wao kimekua mwishoni mwa ligi hizi? Ni mambo ya Freemasons ama ndugu zetu wa kiafrika wanaocheza huko Safari hii wamejiongeza?
 
Kama uchawi wa Waafrica unafanya kazi kwa nn hamna hata nchi moja ya Africa imeweza kuchukua kombe la dunia au hata klabu ya Africa kushinda na kuwa bingwa wa dunia upande wa klabu?
 
Wewe akili yako ndiyo yakichawichawi, ndio maana unawaza uchawi kila kitu!
 
Huenda Hakuna timu ya kiafrika sababu nyingi huwa zinaishia hukuhuku chini kwa kuzidiana nguvu za kichawi
Kama uchawi wa Waafrica unafanya kazi kwa nn hamna hata nchi moja ya Africa imeweza kuchukua kombe la dunia au hata klabu ya Africa kushinda na kuwa bingwa wa dunia upande wa klabu?
 
Mashabiki wa barca na la liga hamuamini kinachotokea. Kutesa kwa zamu champions league.

Miaka 90 mpaka mwanzoni mwa 2000 ligi ya italia ilisumbua hasa ac millan.

2005 2012 ilikuwa ni miaka ambayo ni kawaida kuiona ligi za england fainali ama nusu na wakati kukutana zenyewe.

2012-2018 hapa utawala wa la liga ulikuwa si wa kitoto.

Ila nyakati hizi mambo yanaanza kubadilika kutokana na utofauti ulio mkubwa wa top 6 ya epl na la liga.

Timu sita za juu za epl zina uwezo wa kuaji world class coach na wachezaji wazuri toka sehemu yoyote.

WakTi la liga ni maldrid na barca tu ambazo zimeanza kujichokea.

Hakuna uchawi ila kuna utofauti mkubwa sana kati ya la liga na epl kwa sasa.

Clubs sita za epl zipo kwenye kumi bora ya vilabu tajiri, ilikuwa ni swala la muda tu.
 
Nguvu ya soda hiyo
 

Wewe ndio unawaza hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…