Wachezaji Yanga, Kesho ni Yenu

Wachezaji Yanga, Kesho ni Yenu

Lamisa Danish

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2019
Posts
284
Reaction score
627
Kesho Jumapili tarehe 28 May kwenye dimba la Mkapa inachezwa fainali ya kwanza ya kombe la Shirikisho Afrika baina ya Young Africans hapa nyumbani dhidi ya USM Alger ya Algeria.

Mm kama Mtanzania ninaevutiwa na maendeleo ya soka la Nchi yangu na pia kama Shabiki lialia wa Wananchi,nina jukumu la kutoa mchango wangu hata wa kimawazo tu ili kusaidia mafanikio ya timu.

Niseme wazi kabisa,nina Imani kubwa na viongozi pamoja na bench zima la ufundi likiwa chini ya kocha Nasredine Nabi.Pia nina Imanj kubwa zaidi na Wachezaji wote wa Yanga kwa uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu.

Pamoja na Imani hiyo niliyonayo kwa timu nzima naomba nitoe Rai kwa wachezaji mana hao ndio wenye jukumu zima la kutuletea furaha WanaYanga na Watanzania kwa ujumla.Kesho Jpili ni siku ya kujiwekea historia ninyi wenyewe,ni siku ya kujitangaza ninyi wenyewe,ni siku ya kubadili maisha yenu ninyi wenyewe,ni siku ya kuanza safari kuelekea kilele cha mafanikio yenu ya soka lenu wenyewe.So ni siku kubwa sana kwenu kuliko zote zote mlizowahi kucheza mpira.

Kila mmoja wenu kesho akapambane kwa jasho machozi na damu.kila mmoja wenu akafie uwanjani,kila mmoja wenu atoe kile alichonacho kuhakikisha tunapata matokeo mazuri ya kuelekea fainali ya pili ugenini.Historia ya maisha yenu kisoka inaandikwa kesho.Achaneni na mechi zooote milizowahi cheza ligi kuu,Fa,nk hazina mana saaana kuliko mechi ya kesho ndio mana nikasema ikibidi kufa mkafie uwanjani.

MSITOLEWE MCHEZONI NA KELELE ZA MASHABIKI WATAKAO JAA UWANJANI KUWASHANGILIA,BALI MUWE NA FOCUS, TARGET,CONCETRATIONS YA KILE MNACHOKIFANYA NA KUKIHITAJI ZAIDI AMBACHO NI USHINDI TU PEKEE.

Wachezaji wetu,huwa mna kawaida ya kutoka mchezoni pale mnaposhangiliwa na mashabiki hasa mkipiga chenga or kufanya jambo linalowafurahisha mashabiki,kwa mechi ya kesho kelele hizo msizipe kipaumbele saaana zaidi ya kufocus na LENGO KUU LA MECHI AMBALO NI USHINDI.
Naomba mkacheze JIHAD kama ile mliocheza na Club Africain kule Tunisia,ktk mechi ile niliona kila Mchezaji akipambana akipambania timu na hatimae mechi ile ikawa ndio mwanzo wa ufunguzi wa mafanikio hadi hapa mlipofikia.

Juweni Watanzania wote wenye Akili timamu tuko nyuma yenu,tuko bega kwa bega kuhakikisha kombe tunalichukua,Mh Rais Mama yetu Samia mmeona Juhudi zake tangu awali za kuwahamasisha ili mfanye vizuri zaidi so tafadhalini sana msimuangushe na wala msituangushe pia.

Watanzania wote,tunapenda mafanikio yenu ya kisoka.tunapenda mafanikio yenu ya kimaisha,ndio mana tunawaombea kila wakati ili muweze kutimiza ndoto zenu.Mafanikio yenu ya kimaisha yanategemea kwa kiasi kikubwa na mafaniko yenu ya kisoka na mechi ya kesho ndio ufunguo wa hayo mafanikio so kazi ni kwenu.

Kocha Nabi anaweza kuwapa mbinu zote Nzuri za kufika tunapohitaji ila mwisho wa siku kama mtazembea,kama hamtokuwa serious na mnachokifanya uwanjani mbinu zake zitakuwa hazina mana so kila kitu kimo mikononi mwenu.
Nisiwachoshe sana niwatakie kila lililo la kheri kwenye mechi ya kesho na Mungu aibariki timu yetu tupande ushindi wa goli 3 kwa sifuri Ameen.
 
Kikubwa ni confidence ya wachezaji wasicheze KWA kupaniki watulie as if ni mechi ya kawaida maana huku nje presha ni kubwa sana.Kunaweza kukatokea matukio kutokana na hii mechi.
 
Back
Top Bottom