Wachimba Madini Haramu 100 Wafariki Afrika Kusini

Wachimba Madini Haramu 100 Wafariki Afrika Kusini

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Watu 100 ambao walikuwa wakichimba madini kinyume cha sheria katika mgodi wa dhahabu usiofanya kazi nchini Afrika Kusini wamefariki baada ya kunaswa chini ya mgodi huo kwa miezi kadhaa, huku polisi wakijaribu kuwaondoa huko, kundi linalowakilisha wachimba migodi hao limesema jana Jumatatu.

Sabelo Mnguni, msemaji wa jamii zilizoathiriwa na uchimbaji madini ameliambia shirika la habari la Associated Press kwamba simu ya mkononi iliyotumwa juu ya mgodi huo na baadhi ya wachimba migodi waliookolewa siku ya Ijumaa, ilikuwa na video mbili zikionyesha miili kadhaa iliyofunikwa kwa plastiki chini ya ardhi.

Polisi wanashuku watu hao wamekufa kwa njaa au kwa sababu ya kukosa maji mwilini. Msemaji wa polisi Brigedia Sebata Mokgwabone amesema bado wanachunguza taarifa kujua ni miili mingapi iliyopatikana na ni manusura wangapi waliookolewa baada ya operesheni ya uokoaji kuanzishwa Jumatatu.

SA.jpeg

=================================================================

At least 100 people who were mining illegally in an abandoned gold mine in South Africa have died after being trapped deep underground for months while police tried to get them out, a group representing the miners has said.

Sabelo Mnguni, a spokesman for the Mining Affected Communities United in Action Group, told The Associated Press that a phone sent to the surface with some rescued miners on Friday had two videos on it showing dozens of bodies underground wrapped in plastic.

Mr Mnguni said “a minimum” of 100 men had died in the mine in North West province, where police first launched an operation in November to force the miners out.

They were suspected to have died of starvation or dehydration, he said.

He said 18 bodies have been brought out since Friday.

Source: MSN News/ AP News
 
Dah watu 100 mbona wengi sana na wote hao ni vijana wa kiume
Infact walikuwa ...... zaid ya 200 na wamekaa huko kwa zaid ya miez miwili.. tatizo ilikuwa mwanzon wakigoma kuokolewa wakihofia kupelekwa gerezan moja kwa moja sababu SA walisema wakitolewa wanapelekwa kushtakiwa..

Baada ya mvutano wa haki za binadamu na serikali ya SA ndo govt wakakubali kuwa watawaokoa bila kushtakiwa.. ila ndio hivyo kuna ambao walishakufa.. nakumbuka kuna mmoja alitolewa wakat wanaanza uokozi akadai kuwa sio wote waligoma kuokolewa ila ulilazimishwa kugoma na walikuwa wanazuiwa kupanda kamba ya uokozi
 
Polisi nchi zote wanakuwaga na laana, yaani badala wafikirie namna ya kuwatoa shimoni wao wanatamani wawapeleke gerezani au wafie humo humo.
 
W
Polisi nchi zote wanakuwaga na laana, yaani badala wafikirie namna ya kuwatoa shimoni wao wanatamani wawapeleke gerezani au wafie humo humo.
anadai sababu ni machimbi haram na wengi wai ni wageni ambao hata vibali vya kuishi hawana
 
Back
Top Bottom