Wachimbaji Chunya wafunga barabara ya mwekezaji wakitaka maeneo yao yarudishwe

Wachimbaji Chunya wafunga barabara ya mwekezaji wakitaka maeneo yao yarudishwe

McLaren

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2025
Posts
1,170
Reaction score
3,743
Zaidi ya wachimbaji wadogo 500 wa dhahabu kutoka kitongoji cha Mapele A, kijiji cha Mwaoga Mamlaka ya Mji Mdogo Makongolosi wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wameandamana na kisha kufunga barabara inayoingia na kutoka katika mgodi wa kampuni ya Shanta Mine wakishikinikiza kurejeshewa maeneo yao ya uchimbaji yaliyochukuliwa bila ridhaa yao wala kushirikishwa.

Wachimbaji hao wamemlalamikia Mwekezaji Shanta Mine anayedaiwa kuchukua eneo hilo kwa nguvu likiwa na makaburi ndani yake na kuwataka wachimbaji hao kuondoka bila kuelezwa mahali pa kwenda licha ya kupeleka malalamiko yao kwenye Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chunya.

Miongoni Mwa Wachimbaji hao Wameelezea Historia ya eneo hilo huku wakisema kuna baadhi ya ndugu zao waliozikwa hapo jambo ambalo wameshitushwa Kuona Wanatakiwa Kuondoka Ili Kumpisha Mwekezaji.

Akizungumza kwa njia ya simu Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mbaraka Alhaji Batenga amekiri kuufahamu mgogoro huo na kueleza kuwa ameshaunda tume ambayo itaanza kazi hivi punde.

 
Back
Top Bottom