A
Anonymous
Guest
Wachimbaji wadogo zaidi ya kumi katika eneo la Saza, mkoani Songwe, wanakabiliwa na changamoto ya kuendelea na shughuli zao za uchimbaji wa marudio kutokana na mgogoro unaohusiana na leseni za uchimbaji.
Wachimbaji hao walikata leseni za uchimbaji wa marudio zenye masharti yanayowataka kutochimba zaidi ya kina cha mita nne. Hata hivyo, baadaye leseni nyingine ya uchimbaji ilitolewa katika mazingira yanayoibua maswali kuhusu maeneo ambayo wachimbaji hao walikuwa wakifanyia shughuli zao.
Hali hiyo imewaweka wachimbaji hao katika mazingira magumu, huku wakihisi kukosa msaada wa kutatua changamoto zinazowakabili.
Aidha, siku chache zilizopita vibao vinavyowataka wachimbaji hao kuondoka katika eneo hilo vilibadilishwa. Baadaye, walipokwenda kuchukua mchanga wa marudio, polisi walifika na kuwazuia kuendelea na shughuli zao, huku wakiwaelekeza kwenda kituoni kwa mazungumzo zaidi.
Mkuu wa Wilaya ya Songwe aliwaita wachimbaji hao kwa ajili ya mazungumzo kuhusu changamoto hiyo, mazungumzo hayo hayakufikia suluhisho lililotarajiwa, hali iliyowaacha wachimbaji hao wakiwa na huzuni na wasiwasi kuhusu mustakabali wa shughuli zao.
Inaelezwa kuwa wanaowasumbua wachimbaji hao na kujinufaisha ni baadhi ya viongozi wa wilaya, akimtenga Mkuu wa Wilaya ya Songwe na kueleza kuwa anatarajia mamlaka husika kuchunguza mwenendo wa suala hilo.
Aidha, natoa wito kwa mamlaka za madini na uongozi wa wilaya kutoa ufafanuzi kuhusu leseni, mipaka ya maeneo ya uchimbaji na haki za wachimbaji hao, ili mgogoro huo upatiwe suluhisho la haki.
“USHahidi TUNAO; TUNACHOHITAJI NI HAKI NA SULUHISHO LA MGOGORO HUU"