Wachina 4 wakamatwa kwa utekaji nyara na utakatishaji wa fedha Dar es Salaam

Wachina 4 wakamatwa kwa utekaji nyara na utakatishaji wa fedha Dar es Salaam

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966



Raia wanne wa China, Deng Anqing, Fan Zhong Hua, Zhang Jianjun na Den Qiang wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es salaam wakikabiliwa na mashtaka matatu ikiwemo la kuteka nyara kwa nia ya kudhuru na utakatishaji wa fedha.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao leo Juni 18, 2026 mbele ya Hakimu Mfawidhi, Herieth Mwailolo ambapo Upande wa Mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Judith Kyamba na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Dhamiri Masunde ambapo amedai kuwa kati ya Aprili na Mei mwaka huu, Washtakiwa waliongoza genge la uhalifu lililojihusisha na vitendo vya utekaji nyara na kudai fedha.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka katika Kesi Na. 13626/2026, Washtakiwa wanadaiwa kutenda kosa la uhalifu wa kupangwa kinyume na Sheria za uhujumu uchumi, ambapo waliteka nyara Watu wawili na kudai fedha kutoka kwa waathirika hao. Pia wanadaiwa Mei 15, 2026, katika Mgahawa wa Zhejiang uliopo Wilaya ya Kinondoni, Washtakiwa walijipatia shilingi milioni 130 pamoja na dola za Marekani 70 kutoka kwa mmoja wa waathirika, fedha ambazo walijua au walipaswa kujua kuwa zilitokana na kosa la msingi la utekaji nyara.

Hakimu Mwailolo amesema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo kwa kuwa ni ya uhujumu uchumi, kesi imeahirishwa hadi Julai 2, 2026 na Washtakiwa wamerudisha rumande kwa sababu mashtaka yanayowakabili hayana dhamana.
 
Zihudumiwe familia za wahusika kwanza, ndiyo waendelee kusogeza mbele hizo tarehe zao.
 
Back
Top Bottom