Wachina Kariakoo wanakwepa kodi sijapata kuona

Wachina Kariakoo wanakwepa kodi sijapata kuona

Serikali pia inapaswa kushusha bei ya EFD ili wafanyabiashara wasiwe na sababu ya kupinga kuzitumia. Hili ni swala la msingi. Kama mchakato wa zabuni ktk upatikanaji wake uligubikwa na rushwa au ukiukwaji wa sheria, uchunguzi ufanyike na wahusika wawajibishwe.

Kwa miaka mingi CCM haikutaka Wananchi wajue kuwa wanalipa kodi kila wanaponunua bidhaa. Swala la kuhamasisha ulipaji kodi limeachwa kwa TRA tena ktk msisitizo mdogo. Tunahitaji mapinduzi katika hili.
Watanzania waambiwe kwamba kwa kila sh. 100 inayotolewa kununua bidhaa au huduma Kuna sh. 18 ni hela ya kulipia hosptiali, kujenga barabara, kuleta maji nk. Watu wajue kuwa maendeleo ni Mali Yao. Hiii misemo ya CCM imejenga barabara huku Wananchi wakifichwa Khs uhusika wao na Ujenzi huo zipungue na hata zikome.

kwa maoni yangu mashine za EFD sio za kuuzia wafanya biashara bali wapewe bure kwani watazitumia kuitengenezea malato serikali.

waliozinunua kwa rushwa ili kuwabamiza wafanyabiashara, magufuri atumbue tu majipu hayo
 
Serikali pia inapaswa kushusha bei ya EFD ili wafanyabiashara wasiwe na sababu ya kupinga kuzitumia. Hili ni swala la msingi. Kama mchakato wa zabuni ktk upatikanaji wake uligubikwa na rushwa au ukiukwaji wa sheria, uchunguzi ufanyike na wahusika wawajibishwe.

Kwa miaka mingi CCM haikutaka Wananchi wajue kuwa wanalipa kodi kila wanaponunua bidhaa. Swala la kuhamasisha ulipaji kodi limeachwa kwa TRA tena ktk msisitizo mdogo. Tunahitaji mapinduzi katika hili.
Watanzania waambiwe kwamba kwa kila sh. 100 inayotolewa kununua bidhaa au huduma Kuna sh. 18 ni hela ya kulipia hosptiali, kujenga barabara, kuleta maji nk. Watu wajue kuwa maendeleo ni Mali Yao. Hiii misemo ya CCM imejenga barabara huku Wananchi wakifichwa Khs uhusika wao na Ujenzi huo zipungue na hata zikome.

Tatizo sio.mchina tatizo ni mfumo mbovu wa ccm, ndio ulio tufikisha hapa, imagine katika laki tatu 20 elfu ilikuwa iyende kwa serikali, sasa kwa siku kiasi gani serikali inakosa?
Ni wakati wa kuibana serikali kushughulikia mianya yote ya kutolipa kodi. Vat.
 
Hizi risit mbona zinatofautiana hata layout. Inawezekana huyu mchina anatoa risit fake

attachment.php
 
Tatizo sio.mchina tatizo ni mfumo mbovu wa ccm, ndio ulio tufikisha hapa, imagine katika laki tatu 20 elfu ilikuwa iyende kwa serikali, sasa kwa siku kiasi gani serikali inakosa?
Ni wakati wa kuibana serikali kushughulikia mianya yote ya kutolipa kodi. Vat.

Katika laki tatu kodi ni 54000 sio elf 20. Hawa watu wanaiba Pesa kubwa. Ukiachilia mbali hiyo VAT anakwepa kulipa kodi ya pato maana huwezi jua anaingiza kiasi gani. Sana sana anakadiriwa kodi ndogo baada ya kuhonga au watakokotoa mauzo kulingana na kiwango cha mauzo ambayo ataamua kukatia risiti
 
I wish kila mtu angekuwa anafikiri kama ww ktka maswala ya kodi tungekuwa mbali.
 
Muone kaimu kamishna mkuu wa TRA umpe ili somo na huo ushahidi,naamin unaweza kulikomboa taifa
 
Ndg watz wenzangu,

Siku ya leo Nimeenda kkoo kununua mapazia. Katika pitapita yangu nikapita Duka moja la Wachina liko mtaa wa Aggrey. Nikatoa elfu 80 kulipia mapazia. Yule mchina akinifungia mzigo alafu akapotezea Kutoa risiti. Nikadai risiti.

Alichofanya akaniprintia risiti ya 20000. Nikasema mbona risiti ina kiwango pungufu? Akasema hiyohiyo inatosha. Nikamwambia nataka risiti ya elf80. Msaidizi wake ambaye ni mtz mwenzangu akasema kama vp rudisha mzigo wetu tukupe hela yako. Nikajibu mzigo haurudi na risiti mtatoa. Kuona nimewaka mchina akamtuliza kijana wake akaniprintia risiti nyingine ya elf 60.

Nilichokosea nimesoma tu figure ya mwisho bila kuangalia makato. Kwa kuwa ile ya kwanza ilikuwa na VAT nilidhani na hii iko hivyo hivyo Kumbe haijakatwa hata sh. Moja.

Nimeweka risiti hizi mbili ili mlinganishe. Hiyo yenye TIN inayoishia 49 ni Duka la mtz. Ukilinganisha risiti hizi Kuna tofauti kubwa Naomba wataalam wa kodi na EFD watusadie. Risiti ya mchina ni authentic?

Nimesema Wachina Wanakwepa kodi kwa sababu siku za nyuma kidogo nilinunua Vitasa kwenye Duka Lao nikamprintiwa risiti ya elf70 wakati nilikuwa nimetoa zaidi ya laki tatu.

Nilikomaa akaprinti tena.

Kundi lingine linalokwepa kodi ni wahindi na wapemba. Hawa wanajifanya wameorder EFD Bado hawajaletewa hivyo wanakupa risiti ya zamani. Nimekutana na cases hizi Mara mbili.

Mfanyabiashara anapokwepa Kutoa risiti anakwepa VAT lakini pia anakwepa kulipa income tax kwa sababu kiasi halisi cha mauzo yake kwa mwaka hakiwezi kujilikana.

Tufanye kukomboa taifa kutoka kwenye ufisadi huu?

UPDATE LEO TRH4 DECEMBER

Nimeenda kkoo na kukunua mabegi 6 kwa bei ya sh. 48000. Mchina kama Kawa kaprinti risiti ya 24000. Nikamwambia nataka risiti kamili akaniambia niongeze elf 3000 vinginevyo hatoi risiti nyingine. Nikasema elf 3 ya nini na Wewe umetaja beg ni elf 8 kwa bei ya Jumla kwa piece kuanzia piece 6?. Tukabishana sana akatoa hela Nikasema sipokei hela na ninataka mzigo na risiti kamili. Jamaa kagoma kabisa Nikasema ninakushitaki na nimerekodi maongezi kwenye simu. Akaja mchina mwingine akasema mpe risiti.

Tulipoanza kubishana mchina alijifanya hajui kiswahili, yaani Eti haelewi NENO kodi wala VAT.

SERIKARI ISAIDIE TRA JAMANI KIANZISHWE KITENGO CHA USALAMA WAJIFANYE WANUNUZI ILI WAONE MBINU HII CHAFU NA KUCHUKUA HATUA. This is more than serious yaani Wachina wanafanya wizi bila woga.

Kwa kuwa Rais anaonesha ana Nia ya kukusanya kodi Wtz tuamke tusiadie nchi yetu. TRA na USALAMA WA TAIFA WACHUKUE HATUA KTK HILI. Usalam wa taifa usiwe ni kulinda viongozi tu

Nimetaka kuweka risiti hapa nimeshindwa nitaipost mods wailete hapa
Kwa hio wenye matatizo ni wachina , wapemba na wahindi ? wale wakinga , wachaga , wasambaa na wengine wao wanatoa risiti ?
una mtindio wa kibaguzi. Tatizo hilo ni kubwa Kariakoo na viduka vyote Tanzania. sio kwa kabila fulani
 
TRA waongezewe bajet kubwa ya uhamasishaji hadi watu wengi wajue umuhim wa risit halali. sielewi kwanini kitengo cha matangazo na uhamasishaj huwa kinajikita kubandika makaratas ofisin tu na hali unakuta bajet kubwa imeelekezwa kwa mambo ya UKIMWI ambapo watu wanazika wafu wao na bado hawashtuki gonjwa.
 
Back
Top Bottom