Wachina waenzi asili na utamaduni wao katika ibada ya kumkumbuka Mfalme Huangdi “babu wa Wachina wote”

Wachina waenzi asili na utamaduni wao katika ibada ya kumkumbuka Mfalme Huangdi “babu wa Wachina wote”

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
QQ图片20240422132957.jpg


Ilikuwa ni heshima kubwa mwaka huu kupata mwaliko wa kwenda kuhudhuria ibada ya kumkumbuka Mfalme Huangdi “babu wa Wachina wote”, ambayo ilikuwa kubwa na ya aina yake inayofanyika kila ifikapo tarehe tatu ya mwezi wa tatu kwa kalenda ya kilimo ya China huko Xinzheng mkoani Henan.

Mwaka huu sherehe hii kubwa kabisa ya kumuenzi na kumheshimu anayeaminika kuwa kiongozi wa muungano wa kale wa kabila la Huaxia na mwanzilishi wa ustaarabu wa China, imeangukia Alhamis ya tarehe 11 2024.

Wakati wa utawala wake, Huangdi alilima mazao, aliendeleza uzalishaji, alianzisha uzalishaji wa nguo na nguo za kichwa, na alikuza kilimo na ufugaji wa nondo wa hariri, akiweka msingi wa miaka elfu tano ya ustaarabu wa kale wa China.

Tukiwa tumesimama kwenye uwanja wa sherehe tukiwasubiri viongozi na wageni rasmi, muziki wa jadi ulikuwa ukitumbuiza taratibu huku jukwaa ambalo limewekwa sanamu kubwa la mfalme Huangdi likiwa limefunikwa pazia la rangi ya njano na kusubiri kufunguliwa rasmi wakati sherehe itakapoanza.

Baada ya shughuli kuanza, tukio la kwanza kabisa tuliloshudia kati ya matukio tisa ni kupiga mizinga 21. Baadaye viongozi walipanda kwenye jukwaa kuweka kikapu cha maua wakisindikizwa na askari pamoja na wadada warembo kabisa. Kisha wakachoma uvumba, kuabudu miungu ambapo sote tuliinama mara tatu, kuimba, kucheza dansi, kuiombea China ambapo kulikuwa na dragon mwenye urefu wa mita 75 ili kuadhimisha miaka 75 ya kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China, na maombi ya kuwatakia amani watu, mbingu na dunia.

Nikiwa mgeni pekee niliyebahatika kuhudhuria sherehe hii adhimu iliyojumuisha Wachina takriban elfu tano, ilikuwa ni ndoto yangu ya muda mrefu ambayo hatimye imetimia, kwani mara kadhaa nimekuwa nikisia na kuona kupitia vyombo habari namna Wachina wanavyoenzi mababu zao, katika siku ya kukumbuka watu waliokufa na kufagia makaburi “Qinming” na pia kuthamini urithi wa utamaduni wao kupitia kuendeleza mambo mbalimbali ya jadi.

Wakati tulipokuwa kwenye sherehe hiyo, muziki, mavazi, muundo wa jukwaa na matambiko yote yaliyokuwa yakiendelea uwanjani yaliufanya utamaduni wa kale wa China kuwa hai. Dansi ya Jian Gu, ambayo ni ya kale kabisa ya China na ya kiwango cha juu zaidi cha sherehe katika Enzi ya Han, ilikumbusha upya ustaarabu wa kale ambao umeendelezwa hadi leo, huku wacheza dansi wakipiga ngoma, wakitazamana, wakibadilisha hatua, wakionesha miondoko ya kupendeza huku sauti ya muziki ikitanda angani.

Kwa kuwa hii ni mara yangu ya kwanza kushiriki kwenye sherehe hii ninayoweza kusema ni ya kienyeji zaidi na ambayo kawaida inashirikisha Wachina tu, kwa kweli niliguswa mno moyoni hasa wakati waliporusha njiwa na mabaluni angani, wakiashiria kuenea kwa neema na baraka ambapo muda huo nilishindwa kujizuia na kujiona machozi yakianza kububujika mashavuni.

Katika siku hiyohiyo shughuli hii pia ilifanyika kwenye mtandao wa internet, ambapo Wachina waliopo nje ya nchi nao walikuwa na jukwaa lao la kufanya ibada na kumkumbuka mfalme Huangdi, ambalo lilitumia teknolojia ya AI, VR, na AR ili kuongeza uzoefu wa kuona na mangiliano.

Hili ni tukio adhimu na linalostahili kuenziwa na kuendelezwa na vizazi vijavyo. Halikadhalika natumai kupitia tukio hili sio Wachina tu watakaokuwa na mwamko na moyo wa kurithi utamaduni na kuenzi mababu zetu, bali hata watu wa maeneo mengine pia watathamini mizizi na asili yao, kwa kuendeleza historia yao na utamaduni wao mpana.
 
Wewe dada mchochezi sana

Umeshalishwa propaganda za ki communist basi wewe ukiona mchina unajua wote wako na nia thabiti

Hovyo
 
Back
Top Bottom