Tarehe 8 Agosti ni Siku ya Kufanya Mazoezi nchini China. Siku hiyo, rafiki yangu kutoka Afrika Duncan Likok alisema, “Sasa najua kwa nini China inaweza kupata mafanikio makubwa, kwani ina serikali yenye uwezo mkubwa, na imefanya vizuri kazi kubwa nyingi ikiwemo kutokomeza umaskini pamoja na shughuli za kawaida kama vile kuhimiza watu kufanya mazoezi. Watu wa China kweli wana bahati nzuri sana!”
Duncan ni mwanafunzi wa Kenya ambaye amesoma nchini China kwa miaka mitano. Akizungumzia Siku ya Kufanya Mazoezi nchini China, amesema kinachomshangaza zaidi ni vifaa vya bure vya kufanya mazoezi vinavyopatikana kila mahali kutoka katika bustani hadi makazi, pamoja na umati wa watu wanaofanya mazoezi ya kujenga afya katika bustani na viwanja wakati wa asubuhi na jioni.
Mwaka 2009, ili kuhamasisha watu kufanya mazoezi, serikali ya China iliamua kuweka tarehe 8 Agosti kuwa “Siku ya Kufanya Mazoezi”. Katika miaka 13 iliyopita, miundombinu ya umma ya michezo nchini China imeboreshwa hatua kwa hatua, na kufanya mazoezi ya kujenga afya imekuwa jambo la lazima kwa watu wengi. Katika bustani, wazee wanacheza Tai Chi na dansi, kando ya barabara, vijana wanakimbia kufuatia mpango wao wa kufanya mazoezi uliotungwa na APP ya Simu, kwenye viwanja, watoto wanacheza mpira kwa furaha kubwa wakitokwa na jasho.
China siku zote inazingatia umuhimu mkubwa wa kufanya mazoezi kwa afya ya wananchi wake. Mwaka 2014, China ilichukulia rasmi uhimizji wa kufanya mazoezi kwa watu wote kama mkakati wa kitaifa. Mwaka 2016, “Mpango wa Kitaifa wa Kufanya Mazoezi (2016-2020)” ulitolewa. Mwaka 2017, Mkutano Mkuu wa 19 wa Chama cha Kikomunisti cha China uliweka lengo la “Kuhamaisha Watu Kufanya Mazoezi, Kujenga Nchi yenye Nguvu Kubwa ya Michezo”, na mwaka 2021, China ilitoa Mpango wa Kitaifa wa Kufanya Mazoezi (2021-2025).
Kutokana na hatua za serikali, pamoja na kuboreshwa kwa maisha na mwamko kuhusu umuhimu wa afya, watu wengi zaidi wa China wameanza kufanya mazoezi. Mbali na mazoezi ya kawaida kama vile kukimbia na kucheza mipira, Wachina wengi pia wameanza kufanya mazoezi mapya ikiwemo kuteleza kwenye theluji bandia, Frisbee, na kuteleza katika mawimbi. Haswa baada ya kufanyika kwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, watu wengi walianza kushiriki kwenye michezo ya barafu na theluji.
Kufanya mazoezi kumeleta matokeo chanya. Kulingana na takwimu, asilimia 90.4 ya Wachina wamefikia vigezo vya afya ya mwili, na wastani wa urefu wa vijana wa kiume na wa kike wenye umri wa zaidi ya miaka 19 nchini China unashika nafasi ya kwanza katika Asia ya Mashariki.