Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 977
- 1,966
Raia wanne wa China, Deng Anqing, Fan Zhong Hua, Zhang Jianjun na Deng Qiang, wanaotuhumiwa kumteka nyara mwenzao, wameshindwa kusomewa mashtaka katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Kinyerezi jijini Dar es Salaam kutokana na kukosekana kwa mkalimani.
Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayohusiana na uhujumu uchumi. Hata hivyo, shauri hilo halikuendelea baada ya kubainika kuwa mahakama haikuwa na mkalimani wa kuwawezesha washtakiwa kuelewa mwenendo wa kesi hiyo, kwani hawafahamu Kiswahili wala Kiingereza.
Hali hiyo ilisababisha kushindwa kuendelea kwa hatua ya usikilizwaji wa mashtaka. Hakimu Mkazi Mfawidhi Herieth Mwailolo aliahirisha kesi hiyo hadi kesho ili kutoa nafasi ya kupatikana kwa mkalimani. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha washtakiwa wanaelewa mashitaka yao na shauri linaendelea kwa kufuata taratibu za kisheria.