Wachina waliomteka Mfanyabiashara mwenzao wamkosa Mkalimani wa Lugha

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Your browser is not able to display this video.

Raia wanne wa China, Deng Anqing, Fan Zhong Hua, Zhang Jianjun na Deng Qiang, wanaotuhumiwa kumteka nyara mwenzao, wameshindwa kusomewa mashtaka katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Kinyerezi jijini Dar es Salaam kutokana na kukosekana kwa mkalimani.

Washtakiwa hao walifikishwa mahakamani kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayohusiana na uhujumu uchumi. Hata hivyo, shauri hilo halikuendelea baada ya kubainika kuwa mahakama haikuwa na mkalimani wa kuwawezesha washtakiwa kuelewa mwenendo wa kesi hiyo, kwani hawafahamu Kiswahili wala Kiingereza.

Hali hiyo ilisababisha kushindwa kuendelea kwa hatua ya usikilizwaji wa mashtaka. Hakimu Mkazi Mfawidhi Herieth Mwailolo aliahirisha kesi hiyo hadi kesho ili kutoa nafasi ya kupatikana kwa mkalimani. Hatua hiyo inalenga kuhakikisha washtakiwa wanaelewa mashitaka yao na shauri linaendelea kwa kufuata taratibu za kisheria.​
 
Siyo Wamasai tena kumbe ni Wachina?!Au ni tukio tofauti na La Mchina Mwekezaji kuuawa na kuporwa Milioni 10 kama alivyo tueleza Murilo na sijui alijuaje kiasi Kisha akatutangazia wamekamatwa wakinunua ng'ombe huko mpakani mwa Kenya mnadani?!!?
 
Siyo Wamasai tena kumbe ni Wachina?!Au ni tukio tofauti na La Mchina Mwekezaji kuuawa na kuporwa Milioni 10 kama alivyo tueleza Murilo na sijui alijuaje kiasi Kisha akatutangazia wamekamatwa wakinunua ng'ombe huko mpakani mwa Kenya mnadani?!!?
Hata kama hujasoma habari yenyewe. Kichwa cha habari kinazungumzia utekaji sio mauaji.
 
Nipo naweza hiyo kazi
 
Wangemchukua Chizi Maarifa ana ujuzi wa lugha wa hizo za kichina
 
Wapo wabongo kibao
Wanaozungumza kichina
Hao hawajaamua tu kuwatafuta
Kuna namna hiyo kesi wana I slowdown miezi michache mbele hutaisikia tena

Ova
Una akili za kimjini sana. Hii kwa kiasi kikubwa itakuwa imepangwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…