Wachina watuombe msamaha Waafrika mara moja

Wachina watuombe msamaha Waafrika mara moja

sirjohn

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2014
Posts
767
Reaction score
678
Pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na nchi za kiafrika lakini wachina wanatudharau sana wa Africa.

Wachina wanaita Africa bara la giza/jeusi, bara chafu, bara liloshindikana. Wanaita Afrika FEIZHOU ()非洲) ikiwa na maana dark continent..bara jeusi..

Hiyo ndiyo maana ya FEIZHOU..
Screenshot_2016-11-07-10-27-27-10.png
 
Ni lini omba omba aliwahi kuheshimiwa na kuthaminiwa?
Mawazo ya waafrika walio wengi kuanzia raia hadi viongozi yanawaona wageni (wachina wakiwemo) kuwa ndiyo suluhu ya matatizo yao.
 
kwa swala la high way na
mie nashangaa wajenga maghorofa serikali inawapa wachina wakati kuna wabongo wako vizuri

kwa swala la highway and building construction wachina wako mbali sana..
 
Pamoja na kuwa na mahusiano mazuri na nchi za kiafrika lakini wachina wanatudharau sana wa Africa.

Wachina wanaita Africa bara la giza/jeusi, bara chafu, bara liloshindikana. Wanaita Afrika FEIZHOU ()非洲) ikiwa na maana dark continent..bara jeusi..

Hiyo ndiyo maana ya FEIZHOU..View attachment 430277

Mambo ya kulalamika lalamika haya na maneno maneno hata kama wamesema kweli hayana maana...

Kama deals ziko mezani na zina-benefit then f.uck it,lets do business...biashara haigombi..

Zamani ni Egyptians,wakaja Wagiriki,wakaja Roman Empire,wakaja Wazungu,wakaja Wamarekani,watakuja Wachina then Wahindi most probably tukafatia Waafrika....muda wetu utafika hata kama ni 1000 yrz to come...

Waache waringe,it don bother us as long as biashara ina make sense,kama hamna maslahi hata watupende vipi I cant do business wit'em!
 
Kwa sasa ni kweli labda mambo yabadilike mbeleni.
 
Kosa lao ni kusema ukweli katika hii Dunia ya kupakana mafuta kwa mgongo wa chupa.
 
Hiyo tamko wameitoa serikali ya China??

Au umekutana nayo mtandaoni mtu kajiandikia tu

Tuanzie hapo kwanza
 
Nilifanya utafiti wangu kupitia magazeti ya kampuni mbili tu kwa miezi mitano, nilikuja kugundua raia wa nje wanaongoza kwa kufanya jinai ni hawa chini hizi ni habari zilizoripotiwa tu na vyombo viwili tu

1.Mchina afikishwa kortini kwa kukwepa kulipa kodi mwenye kampuni ya HM Textile Co Ltd iliyopo mtaa wa Agrey kariakoo, Hui Fang Ma, aukumiwa kwenda jera miaka miwili au kulipa faini ya milione nne, alipa faini. Mwananchi 23/03/16.

2. Wachina wafikishwa kortini kwa kukwepa kulipa kodi, Liu Song Yue, Liu Peng Fey na Jiang Zendog wenye duka lilipo Tabata, wahukumiwa kwenda jera miezi sita au kulipa faini ya milioni nne, walipa faini. Mwananchi 12/4/16.

3. Mkuu wa mkoa Morogoro kaka kakamata wachina wawili kwa kuendesha mgodi wa Marumaru kinyume na sheria na kukwepa kulipa kodi ya milioni tisini na mbili mil 92, cha Zhan Fa construction material Group Ltd. Mwananchi 17/4/16.

4. Mchina Bui Hao jera miaka ishirini kwa kukutwa na meno ya simba na kucha. Tanzania Daima, 20/4/16.

5. Wachina wawili wafikishwa mahakamani kwa kukwepa kulipa kodi, wenye kampuni ya Dong Shen International mtaa wa Narung'ombe Kariakoo. Pai Shu Chea na Apple Chen, wahukumiwa kwenda jera miaka mitatu au kulipa faini milioni mbili kila mmoja, walipa faini, Mwananchi 20/4/16.

6. Wafanyakazi wa Kampuni ya China Railway Jiangchan Engineering Ltd (CRJE) wanaojenga Hoteli ya NSSF Mwanza wagoma kwa kulipwa pesa pungufu na kunyanyaswa. Tanzania Daima 15/4/16.

7. Jumuia ya wafanyabiashara Tanzania (JWT) yalalamika kuhusu wafanyabiashara wa kichina Kariakoo. Mwananchi 14/4/16.

8. Wachina mbaroni kwa kutaka kutorosha noti za mia tano zenye thamani ya milioni therathini, noti sitini elfu (60,000) Su Ning na Feng Guang Quan. Mwananchi 31/3/16.

9. Wachina wanaofanya kazi Hospitali ya Taifa Muhimbili (Chinese medical team) wanaswa wamejiunganishia maji ya DAWASA Oysterbay mtaa wa Mtwara. Watozwa faini ya milioni kumi na saba, (17) wanatakiwa kulipa faini ndani ya kipindi cha miezi ishirini na nne, (miaka miwili) Tanzania Daima 21/3/16.

10. Wachina wawili Xu Fujie na Huang Gin waliyokamatwa na meno ya Tembo mia mbili ishirini na sita (226) wafungwa jera miaka therathini au kulipa faini bilioni mia moja na nane (208) waenda jera, Mwananchi 9/3/16.

11. vigogo laki tatu (300,000) wa chama cha kikomunisti China (CCP) kinachotawala China wafungwa kwa ufisadi. Mwananchi 9/3/16.

12. STAMICO yaingilia mgogoro wa wachina na wafanyakazi wake kuhusu mikataba na maslahi ya wafanyakazi wa kampuni ya China Civil Engineering construction corporation, wanaofanya kazi hospitali ya Taifa Muhimbili, Mwananchi 1/3/16.

13. kampuni ya Tanzania China Trade and Tourism development Ltd ambayo ni waagizaji wa pikipiki aina ya Falcon. Wakamatwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kutengeneza namba za pikipiki na magari bila kuwa na kibali cha TRA cha kufanya hiyo kazi kinyume cha cha sheria, mkurugenzi mkuu Donglinh Guo, meneja wake Yong quing Chen na mtunza stoo Peng Zhan. Waleta fujo wakati wa kukamatwa kwao. Tanzania Daima 9/2/16.

14. Wafanyakazi wa kampuni ya Ocean kiss walalamika kwa kupata mshahara mdogo, kunyanyaswa na kukatwa mishahara elfu ishirini wanapochelewa. Tanzania Daima 9/2/16.

15. Wafanyakazi zaidi ya mia mbili (200) wa kampuni ya China railway Jiangchang engineering (CRJE) wanaofanya mradi wa daraja la kigamboni wagoma kwa kupunjwa stahiki zao. Tanzania Daima 16/2/16.

16. Wachina kumi na sita (16) wakamatwa Geita wakiwa wanachimba madini na viza ya utalii, Mwananchi 18/2/16.

17. Wafanyakazi mia mbili (200) wa Chima Hainan International Co. (CHICO) wanaotengeneza barabara ya Kyaka - Bunene. Wagoma walipwe malimbikizo yao ya mishahara na kunyanyaswa. Mwananchi 6/3/16.

18. Kampuni ya Kichina StarTime inayojishughulisha na huduma za vigamuzi yakamatwa na simu elfu mbili mia saba orobaini na nne, (2744) zisizo lipiwa kodi. Mwananchi 3/2/16.

19. China ni kinara wa wahamiaji haramu nchini, wakamatwa mia mbili themanini na tano kwa siku sita tu. (6) Kuanzia February 8-14. mwananchi 25/1/16.

20. Wachina wanaswa wakiiba maji, ni kampuni ya Allied Transportation inayotengeneza mabati iliyoko maeneo ya Buguruni. Tanzania Daima 25/1/16.

21. Polisi wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro wanamlinda raia wa china mwenye kiwanda cha Mega copper anayefyatua risasi hovyo kutisha wananchi. Mwananchi 20/1/16.

22. Wafanyakazi wa mia tatu na sitini (360) wa kichina wa kiwanda cha Dangote Mtwara wakamatwa kutokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini. Mwananchi 10/1/16.

23. Naibu waziri wa mazingira afuta kibali cha kiwanda cha Dhahabu Mbeya cha Sunshine Mining cha wachina kwa kushindwa kutimiza vigezo na kuchafua mazingira kwa kiasi kikubwa. Mwananchi 10/1/16.

24. Mchina mbaroni kwa kukutwa na meno ya Ngiri uwanja wa ndege Dar es salaam, Mwananchi 5/5/16.

25. Naibu waziri afungu kiwanda cha S & Y Co. Kutokana na mazingira' kutokuwa salama na kuwa na wafanyakazi wengi wasiokuwa na vibali zaidi ya kumi (10) cha kutengeneza mbao nyepesi, Mwananchi 7/5/16.

26. Kiwanda cha sunshine Industry cha Dodoma kinachozalisha mafuta ya Alizeti kina wafanyakazi wengi ambao hawana vibali vya kufanya kazi nchini. 7/5/16.
 
wavimba macho,.jamaa ni waalifu ajabu,yaani mpaka vibabu vya kichina noma
 
Back
Top Bottom