Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Katika hatua ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, wachoma nyama mkoani Arusha wameahidiwa kupewa majiko yanayotumia nishati safi kwa ajili ya kazi yao.
Hayo yamesemwa leo Ijumaa Machi 7, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda wakati akikagua maandalizi ya nyama choma kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo kitaifa yatafanyika jijini hapa kesho Machi 8.
Makonda amesema miongoni mwa sababu ya athari ya mabadiliko ya tabianchi ni ukataji holela wa miti kwa ajili ya shughuli za kibinadamu ikiwamo uchomaji mkaa, hivyo ofisi yake itagawa majiko ya nishati safi ili kukabiliana na hilo.