Wachuja Nafaka Na Albamu Yao Kali Kuwahi Kutokea Tanzania

Wachuja Nafaka Na Albamu Yao Kali Kuwahi Kutokea Tanzania

Dr am 4 real PhD

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2016
Posts
11,640
Reaction score
24,066
images (65).jpeg


WACHUJA NAFAKA Tusisubiri Wapotee wote.....ndiyo tuseme waliwahi kutoa Moja ya Albamu kali, Narudia Tena Albam kali kuwahi kutokea Tanzania.

Fatilia Uzi Huu utajua kwanini nakuambia Ilikuwa moja ya Albam Kali Tanzania.

WACHUJA NAFAKA lilikuwa kundi la Muziki wa RAP lililoundwa na wasanii Juma Nature, KR na Dollo mzee wa Ladhia, Wote hao wakiwa ni wasanii kutoka Wilaya ya TEMEKE moja ya Wilaya yenye historia kubwa na muziki wa Tanzania enzi Hizo

Albam ya Wachuja Nafaka ilitengenezwa chini ya Label Kubwa na yenye heshima kubwa sana kwenye tasnia ya Muziki wa Tanzania BONGO RECORDS chini ya P FUNK Majani, kwahiyo kuhusu suala la Productions siyo la kutilia shaka.

Ni albam iliyokuwa na Nyimbo Tisa za Moto sana, Kuanzia ubora wa Beats, Ubunifu kimashairi, Korasi zilizoimbwa humo, na Ujumbe ambao ndicho kilikuwa kitu kikubwa sana kwa kipindi hiko na soko lilikuwa likiwapa nafasi zaidi watu wanaoandika ujumbe.

COLLABO YA KIMATAIFA Kwenye Albam hii ya Mzee wa Busara kuna wimbo wa Mapato ambapo kuna Collabo ya mnyama Bamboo, alipita humo moja kati ya Rappers wakali sana kutoka Kenya miaka hiyo

Wachuja nafaka Ndio walimuibua FID Q baada ya kumsikia mwanza na kumtabilia makubwa. Kwenye hii albam FID Q Ali ibuliwa na Alishirikishwa kwenye wimbo mmoja kama underground ila akaja kua msanii mkubwa bongo.

Kumbuka kwenye Albam hiyo ni ngoma tatu pekee kati ya Tisa ndizo walikuwa wameshirikishwa watu wengine, ile ya Bamboo, Inspector kwenye mzee wa Busara na FID Q ambaye alikuwa bado Kinda kwenye muziki ila wao walishauona ukali wake mpaka kumpa nafasi.

Yani ngoma za kwenye Albam hii zilikuwa za moto kiasi kwamba takribani nyimbo 7 zote zilipotoka ziliwahi kuwa kwenye Top10, Top5 za Radio na Zile Chart za kwenye magazeti (Wazee wenzangu mnazikumbuka)
 
Wachuja nafaka
Kwangu kwako tanooo
Wachuja nafaka
Haina mfano
Wachuja nafaka
Mpaka utadataa

Hahahahahaha enzi hizo kina Doro, Nature
 
Back
Top Bottom