Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Ukisoma kwenye magazeti, ukienda kwenye mitandao mbalimbali, wanaume ndio wanaongoza kwa kutafuta wachumba. Sababu nini hasa?
Hili linahitaji takwimu ili kupata uhakika kwani mimi nadhani ni kinyume chake nikiwa na maana wanawake ndio wanaongoza kutafuta wenza wao hasa kwenye mitandao.
Nidhaniavyo mimi sababu ni nyingi na hapa nitaongelea kijumla (wanawake na wanaume). Kuna wanaoenda kwenye mtandao ili waweze kuibia. Mtandao unarahisisha sana watu kuwasiliana. Fikiria hata humu, wote tuko hapa lakini tumetawanyika kila pande ya dunia. Sasa kama mtu anataka kuibia na yuko mji A, ili kurahisisha azma yake anaingia kwenye mtandao na kutafuta mwenza kwenye mji B ambako chances za kubambwa zinakuwa ndogo.
Pia, mtandao umepanua wigo. Kabla ya mtandao ilikuwa vigumu sana kukutana au kuwasiliana na watu walio mbali. Lakini siku hizi hata mtu awe wapi, uko one click away kuwasiliana na huyo mtu. Hata hela unaweza ukatuma bongo kwa mfano na katika dakika chache tu zikawa zimefika. Kwa hiyo mtandao kwa namna ingine umerahisisha makutano ya watu.
Tatu, inakuwa ni rahisi kwa kiasi flani kum-screen mtu. Hebu fikiria uko kazini halafu kuna njemba imekuzimia na kila siku inakughasi ghasi lakini wewe haui-feel kihivyo. Si itakuwa jinamizi kila siku uendayo kazini? Sasa kwenye mtandao unaweza angalau ukamtosa mtu kiurahisi kama unaona anakuboa ingawa huwezi kujua kwa uhakika kabisa huyo mtu yukoje ana kwa ana. Mtandao unarahisisha mchakato wa mwanzoni katika kujuana. Mtaulizana maswali lukuki na msipopendezewa na majibu basi kila mtu anakitoa kivyake bila hofu ya kuwa stalked unless ulitoa information zako kuliko inavyotakiwa.
Kuna baadhi ya akina dada wanasema kuwa wametafuta wenza wao weee-makazini, mashuleni, kwenye mabaa, kwenye maklabu, kwenye vituo vya kujazia mafuta, kwenye stendi za mabasi, maktaba, n.k. lakini wapi...hawabahatiki kupata yule wanaemtaka. Matokeo yake wana test zali kwenye mtandao. Wapo wanaobahatika na wapo wanaoendelea na hiyo bahati yao mbaya.