Wachumi mtujuze Je, DHAHABU inatunza vipi sarafu au shiling ya nchi?

Wachumi mtujuze Je, DHAHABU inatunza vipi sarafu au shiling ya nchi?

AI BRAINFULL

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2019
Posts
2,122
Reaction score
5,319
Hua sielewi dhamani ya dhahabu kua kubwa duniani na kuheshimika kuliko madini yoyote hasa SERIKALI za duniani kutumia na kuamini kua ndio mkombozi,mbadala na kinga ya msukosuko wa uchumi dunia
 
Hua sielewi dhamani ya dhahabu kua kubwa duniani na kuheshimika kuliko madini yoyote hasa SERIKALI za duniani kutumia na kuamini kua ndio mkombozi,mbadala na kinga ya msukosuko wa uchumi dunia
Ni thamani sio dhamani,
Halafu sio kwa sababu bei ni kubwa tu bali kwa sababu bei yake haibadiliki sana, haiharibiki na ni madini adimu yanayobadilishika kirahisi kwa fedha sehemu kubwa ya dunia.
 
Ndio walivyoamua wazungu kuwa dhahabu iwe mbadala wa fedha ikiwa kutatokea dharura ya uhitaji

Algeria wamehifadhi ton 174 na wanaongoza Africa
Sisi Magu alijaribu kuweka na tulikuwa na tani 9 mkaziuza
Yaani mmeuza akiba ya Taifa tena tutani tisa 🤔

Hata wewe ukiwa na hela za ziada nunua dhahabu ficha utaiona thamani yake Baada ya miaka kadhaa
 
Anavyoamua beberu wewe unafuata, Nyerere alisema hata "bei ya korosho anaamua mzungu", statement inabeba uzito sana hiyo.
 
Ni kwa sababu ya Mambo ya kiroho ya uchumi wa sehemu hiyo.....

Movie ya Money heist episode ya mwisho kuna ujumbe mzuri baada ya professor kubadiri Gold reserve ya nchi ya vipande vya Dhahabu kwa zile gold painted cans za chakula.
 
Tajiri, kichumi ni kwamba nchi zetu hizi zinahitaji reserve ya $ na TSh kwenye mzunguko kwa uwiano. $ ikiwa haipo ni tatizo, na $ hiyo hiyo ikizidi ni tatizo, ina madhara (ndio hapo unaona shilingi inashuka dhidi ya $), au utasikia $ imeadimika, haipo kwenye mzunguko. Sababu ni kwamba sisi tunagemea $ kwenye mzunguko wetu. Hii inaitwa "Dollar dependence".

Sasa, serikali lazima ihakikishe ina reserve ya $, na $ ipo kwenye mzunguko kwa uwiano. Sasa inakuwaje serikali. Kupitia benki kuu, inanunua/inaweka reserve ya GOLD.
Kupitia maelezo hayo, sasa tuyatumie kupata majibu ya swali lako;

Lengo la kuu ni kupunguza utegemezi wa dola. kuhakikisha dola haizidi kwenye mzunguko wala haipungui, kulinda thamani ya fedha ya ndani na mfumuko wa bei. kununua GOLD, Maana yake unahifadhi shilingi kupitia GOLD ili uje uuze kwa dola. Hivyo kui regulate $ kwenye mzunguko na kupunguza utegemezi wa $ ambao una madhara hasa mfumuko wa bei (Inflation). Ni rahisi sana ku regulate dola, ukiwa na GOLD uliyonunua kwa Shilingi. Sababu ni kwamba unapohitaji $ unauza GOLD kwa dola, na ambapo huitaji $, unakusanya GOLD kwa shilingi. 😊

DOLA ikizidi ina madhara na ikipungua pia ina madhara kwa uchumi. Ukiacha dhahabu yote inunuliwe kwa $, maana yake $ iwe nyingi. Ndio maana serikali inatumia shilingi yake kununua GOLD, ili badae iuze kwa dola inapozihitaji. Kwa kufanya hivyo tunasimamia mfumuko wa bei na thamani yq shilingi yetu dhidi yq dola.

Mkakati huo una faida nyingi sana, kwani dhahabu % flani inabaki ndani, dola zinabaki ndani hazitoki nje.
Pia ni biashara, sababu soko la dhahabu huwa lina swing, Gold huwa inapanda bei, na dhahabu iliyokusanywa inauzwa.

NOTE: Dhahabu unanunuliwa kwa shilingi sio dola. Inakuja kuuzwa kwa dola.
 
Algeria wamehifadhi ton 174 na wanaongoza Africa
Sisi Magu alijaribu kuweka na tulikuwa na tani 9 mkaziuza
Yaani mmeuza akiba ya Taifa tena tutani tisa
🤔

Hata wewe ukiwa na hela za ziada nunua dhahabu ficha utaiona thamani yake Baada ya miaka kadhaa
Babu bado unashangaa matukio ya nchi yetu yenye amani, watu wengi wa ulaya wanaililia sana😂
 
Ni kama movie ila ndio imeisha hiyo, mimi nasubiri mgawanyo wa bil mia saba ninunue hata ac kwaajili ya joto la el nino! Kama ni madogo washamaliza necta so far hakuna hasara kwa taifa! Turudi majumbani..
Kama ni mgao naona utasubiri sana
Watu wameisha kuja NY na Paris na London kufanya shopping 😂
Na madogo hao muwatunze kwa maadili jamani wawe Taifa bora la kesho
Ila hilo joto nalo vumilia kwa sasa hakuna jinsi
 
Kama ni mgao naona utasubiri sana
Watu wameisha kuja NY na Paris na London kufanya shopping 😂
Na madogo hao muwatunze kwa maadili jamani wawe Taifa bora la kesho
Ila hilo joto nalo vumilia kwa sasa hakuna jinsi
Aiseee shopping ya nini tena😁

Tuko makini, sema kila mtu amlinde mwanae tu! Maana malezi kwa makundi ni uongo kwa kizazi hiki! Dah wacha nivumilie tu tafanyaje sasa🙁
 
Aisee nchi ni ngumu hii! Mitaani watu wanavyolia shida, maisha magumu, ajira hakuna! All they can do ni kujiangalia na kujigawanisha kama wanaishi mji mmoja!
Hali ngumu Kweli Ila tatizo nchi nyingi Africa hazijitambui kabisa na viongozi wanaona sawa tu
 
Back
Top Bottom