Wachumi naombeni Elimu juu ya uhusiano ufungaji wa maduka ya kubadili fedha na uhaba wa fedha za kigeni nchini

Wildlifer

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2021
Posts
1,884
Reaction score
5,235
Ninasikiliza DW hapa, kuna bwana mmoja anasema,
"kufungwa kwa Maduka hayo mtaani kumepekea bei ndani ya mabenki kuwa kubwa, pia anasema dola ipo mtaani tatizo watu wanashindwa kuzibadili sababu ya bei ndogo kwenye mabenki." so anashauri maduka hayo yafunguliwe.

Nijuavyo mimi dola hupungua sababu ya low export au manunuzi makubwa nje ya nchi ambayo hutumia dola.

wachumi, nipeni mwanga.
 
Inawezekana labda kuna baadhi ya watu wanazo mikononi (fedha za kigeni),hawajaziruhusu kwenda kwenye mzunguko/ kuuzia mabenki au maduka ya kubadilishia fedha.​
 
Tatizo la uhaba wa dollars linakuzwa sana utadhani lina athari. Kwanza tuanzie hapa; Kwanini watu wanataka kununua dollars?
 
Manunuzi /safari zote za nje zinahitaji fedha za kigeni; na pale zinapokosekana ndipo suala la kukopa linapokuja.
 
Mdogo wangu ana akaunti ya Tsh pale CRDB na anafanya biashara ya spare part za pikipiki na generators.

Mwaka jana mwezi September alisafiri kwenda Gwangzhou na Visa Card yake kutoka CRDB Bank.

Kabla ya safari alikwenda branch yake akawaambia anasafiri kwenda kufunga mzigo wa kama USD 20,000 (sawa na Tsh 50 Million).

Walichofanya wakamuongezea limit ya ku-draw ATM akiwa kule Guangzhou. Dogo alisafiri na akafunga mzigo bila kununua dola hata moja. Alinunua mzigo kwa Chinese Yuan.

Nashangaa wasio na mahitaji ya dollas ndiyo wanalalamika kuwa dollas hazipo na zikipatikana bei iko juu
 
Mdogo wangu ana akaunti ya Tsh pale CRDB na anafanya biashara ya spare part za pikipiki na generators...
Dolla ni standard katika kubadilishana, maana yake popote inakubalika; ata ukienda zimbabwe utanunua vitu kwa ela ya zimbambwe, sasa kama huna ela ya zimbabwe, itakulazimu utumie dolla kwenda ela ya zimbabwe.

Hata mzungu anapokuja hapa kwetu, atatumia ela yake (dolla au euro n.k) na kuibadilisha ili apate ela ya kwetu ili aweze kufanya matumzi yake.​
 
Tatizo la uhaba wa dollars linakuzwa sana utadhani lina athari. Kwanza tuanzie hapa; Kwanini watu wanataka kununua dollars?
Kumbe hata hujui kwanini wanazitaka dola alafu unasema watu wanakuza mambo?

Hiyo simu yako ya tecno unadhani kana sio dola ungekaa uione bongo?
 
Dolla ni standard katika kubadilishana, maana yake popote inakubalika; ata ukienda zimbabwe utanunua vitu kwa ela ya zimbambwe, sasa kama huna ela ya zimbabwe, itakulazimu utumie dolla kwenda ela ya zimbabwe.

Hata mzungu anapokuja hapa kwetu, atatumia ela yake (dolla au euro n.k) na kuibadilisha ili apate ela ya kwetu ili aweze kufanya matumzi yake.​
Ela ndiyo nini sasa? Wengine muko JF ila hamjasoma hata ngumbaru!! Mtatusumbua sana
 
Kumbe hata hujui kwanini wanazitaka dola alafu unasema watu wanakuza mambo?

Hiyo simu yako ya tecno unadhani kana sio dola ungekaa uione bongo?
Ukiwa na akili kisoda huwezi kunielewa!! Wewe soma tu ueleweshe
 
Mdogo wangu ana akaunti ya Tsh pale CRDB na anafanya biashara ya spare part za pikipiki na generators.

Mwaka jana mwezi September alisafiri kwenda Gwangzhou na Visa Card yake kutoka CRDB Bank.

Kabla ya safari alikwenda branch yake akawaambia anasafiri kwenda kufunga mzigo wa kama USD 20,000 (sawa na Tsh 50 Million).

Walichofanya wakamuongezea limit ya ku-draw ATM akiwa kule Guangzhou. Dogo alisafiri na akafunga mzigo bila kununua dola hata moja. Alinunua mzigo kwa Chinese Yuan.

Nashangaa wasio na mahitaji ya dollas ndiyo wanalalamika kuwa dollas hazipo na zikipatikana bei iko juu
Hakununua kwa Yuan. Alinunua kwa dola. Dola zikiingia kwenye serikali ya China.
 
Mbona unaleta ubishi wa kijijini? Mimi mwenyewe nimesafiri sana nilipokuwa corporate staff. Kila shopping nilikuwa nafanya kwa viza card iwe Dubai, Johannesburg au London. Nikiwa JOBURG nikitaka hard cash, nina draw inanipa South African Rand

Kama hujui Visa Card inavyofanya kazi uliza uelezwe
 
Mambo.

Wanachofanya wanachukua hela yako wanaibadili kwenda kwenye dola kwanza halafu wanachukua dola wanabadili kwenda kwenye hela yao. Hapo unakuta umekatwa hela maradufu na exchange rate ni kubwa sana.

Nilitumia account ya CRDB nikatoa XOF hayo makato na exchange ni balaa.
Nikatumia account ya dola ya EXIM kutoa hela makato yakawa madogo.

So hakuna direct exchange kaa chini upige mahesabu vyema.
 
Kama Benki kuu ina akiba ya Yuan, transactions China zitakuwa in Yuan as long as Benki kuu na hiyo benki unayoitumia zina makubaliano.
Pia unaweza kutumia USD au EURO kununua vitu kama unayo akiba yenye fedha hizo personally. China kwa mfano, hununua dollars na Uuros hata kama interest rate ya USD ni 1% and sometimes -1% kwa sababu ni fedha stable na zinatumika nchi nyingi. Hii haimaanishi kuwa hutumii yuan directly ila wananunua USD lakini hawanunui Yuan kwa hiyo ukiwa na USD ni kama unaiuza.
Ndiyo maana watu wanasema China anamkopesha USA, kumbe ananunua bonds kwa wingi hata zikiwa na very low interest saa nyingine in negatives hivyo kuhodhi deni la US.
 
Ninasikiliza DW hapa, kuna bwana mmoja anasema,
"kufungwa kwa Maduka hayo mtaani kumepekea bei ndani ya mabenki kuwa kubwa, pia anasema dola ipo mtaani tatizo watu wanashindwa kuzibadili sababu ya bei ndogo kwenye mabenki." so anashauri maduka hayo yafunguliwe.

Nijuavyo mimi dola hupungua sababu ya low export au manunuzi makubwa nje ya nchi ambayo hutumia dola.

wachumi, nipeni mwanga.

Kwani wakati yapo ulisikia hakuna dollar?
 
Ninasikiliza DW hapa, kuna bwana mmoja anasema,
"kufungwa kwa Maduka hayo mtaani kumepekea bei ndani ya mabenki kuwa kubwa, pia anasema dola ipo mtaani tatizo watu wanashindwa kuzibadili sababu ya bei ndogo kwenye mabenki." so anashauri maduka hayo yafunguliwe.

Nijuavyo mimi dola hupungua sababu ya low export au manunuzi makubwa nje ya nchi ambayo hutumia dola.

wachumi, nipeni mwanga.
Kwani Magu bado anatawala nchi hii?
Si walisema aliyafunga na wakayafungua? nini sasa hiki
 
Shida kila kitu kipo kisiasa, wanaopiga kelele sijui dolar imekuaje wala si watumiaji, ni mkumbo tu na ushabiki wa kisiasa
 
Back
Top Bottom