Ningependa kupewa ufafanuzi wa kiuchumi ni hali ipi huwa ina unafuu
A. Mzunguko wa pesa kuwa mdogo ila bei za bidhaa / huduma ni kawaida.
B. Mzunguko wa pesa kufufuka ila bei zinakuwa zimepanda
Kwa hapa Tanzania, tunapitia mengi zaidi ya mzunguko wa pesa na inflation.
Unatakiwa pia ufahamu ni nini huwa kinasababisha inlation, na nini kinasababisha mzunguko wa pesa kuwa mkubwa au mdogo.
Hali ya sasa inachangiwa na mambo makubwa manne:
1) Uchumi uliharibiwa sana wakati wa awamu ya 5, kiasi cha kuondoa pesa nyingi sana kwenye mzunguko:
= kwa sababu ya kugandamiza demokrasia na haki za watu, tulifutiwa pesa ya MCC zaidi ya sh 1.4 trillion, tuliyokuwa tunapata kila mwaka, pesa ya bure siyo mkopo, yenye masharti makubwa mawiloli, nchi iheshimu haki za binadamu na demokrasia.
Pesa hii ilikuwa inatoka nje na kuingia nchini, ikiongeza mzunguko wa fedha, ajira na akiba ya fedha za kigeni, kwa ujinga tu, tukaipoteza. Tulikuwa tunapewa nchi 2 tu, Tz na Ghana katika bara la Afrika.
- Kutokana na utawala wa kidikteta, mataifa yanayochangia bajeti ya maendeleo yalipunguza mchango wake kwa zaidi ya 50%. Mpaka sasa, michango yao haijarudi kufikia ilipokuwa kabla ya kupunguza.
= Kutokana na sera mbaya za uchumi, kodi na uwekezaji, makampuni zaidi ya 500, ya ndani na nje, yaliondoka Tanzania. Haya maana yake yalipunguza pesa iliyokuwemo nchini na iliyokuwa inaingia nchini.
= mbaya zaidi baada ya kuvuruga uchaguzi wa 2020, na kutokuwa na kambi rasmi ya upinzani bungeni, tukakosa sifa ya kupata msaada wa zaidi ya trilioni 1 3 toka Jumuia ya Madola. Walipokuja kushtuka kuwa wataikosa hii pesa kutokana na ushenzi uliofanyika kwenye uchaguzi, zilifanyika jitihada kubwa za kutaka wapinzani waingie bungeni, lakini walikuwa wamechelewa, mbinu zote zikagonga mwamba, covid 19 hawakusaidia kitu kwa sababu hawawezi kufikia 14% ili wawe na sifa ya kuunda kambi rasmi ya upinzani kama sheria inavyotaka.
Mambo haya yaliondoa pesa nyingi sana kwenye mzunguko.
2) Kupungua kwa uwekezaji. Uwekezaji, hasa wa nje, huwa unaleta mitaji kutoka nje. Wakati wa awamu ya 5, ukuuaji wa uwekezaji uliporomoka kutoka 28% mpaka 4%.
3) Kupungua kwa kiasi kikubwa kwa mauzo ya nje. Thamani ya mauzo ya nje ya mazao, wakati wa awamu ya 5 yaliporomoka kwa 50%, mpaka leo, hali haijarudi kufikia mahali tulipokuwa. Hali hiyo pia ulizikumba sekta nyingine kama za utalii na madini. Japo absolute nambers zilionesha kuna ongezeko lakini kulikuwa na poromoko kubwa katika ukuuaji.
4) Kupanda sana kwa gharama za uzalishaji kulikochangiwa na covid 19 na vita vya Ukraine. Covid 19, kwetu sisi kwa kiasi kikubwa kulitusaidia sana kwenye mafuta. Bei ya mafuta ilidondoka kwa zaidi ya 50%, na hivyo kufanya uzalishaji wa ndani na usafirishaji unaotegemea nishati ya mafuta, kuwa nafuu sana, japo bei za bidhaa za kutoka nje zilikuwa juu. Hali ikabadilika sana baada ya vita vya Ukraine iliyosababisha bei ya mafuta kupanda maradufu, na hivyo kupandisha bei ya kila kitu.
Mwisho, tunachokiona sasa, kina mchango mkubwa sana wa utawala uliotangulia. Kwa sababu zile pesa za msaada za bure hazipo, wanalazimika kukopa sana. Wawekezaji wengi walioondoka wakati wa awamu ya 5 hawajarudi, na wengine hawatarudi tena.
Uchumi kuuharibu ni rahisi sana, uharibifu unaweza kufanyika hata kwa mwezi mmoja tu, lakini kurekebisha inaweza kuchukua zaidi ya miaka 10. Yanayofanyika sasa, madhara yake, yawe positive au negative, tutaanza kuona zaidi kuanzia miaka mitano ijayo.
Kwa kawaida, inflation haijawahi kusimama ila hutofautiana katika viwango. Inflation siyo mbaya kama mzunguko wa pesa ukiwa mzuri.
Kwa sasa wengi wanashuhudia hali ngumu kwa sababu kuna yote mawili, inflation ipo juu, na mzunguko wa fedha bado upo chini.