Wachumi, ni wapi pana nafuu kati ya awamu ya tano na ya sita?

Upupu kabisa huu.. yaani anakopa ili kulipa madeni
 
unategemea kuwe na mvua ya pesa ? ingia mtaani kapige kazi mkuu
Hebu nipe mfano wa kazi unayohisi italeta mzunguko wa pesa au unakaza fangasi na ukoma kuandika kitu usicho na uelewa nacho.


😂😂😂 Mtaani kapige kazi
 
Siku zote ukiona pesa inazunguka ujue Kuna fursa ila ukiona hali ya mzunguko wa pesa ni mdogo vitu bei Chee ujue Kuna umaskini uliotopea..

Takwimu kama hizi ilikuwa nadra sana kuzisikia awamu ya Jiwe zaidi ya maigizo ya magawio na upuuzi mwingine
 
Leta mfano wa hizo bank na kiasi cha hizo riba
Wewe unaishi nchi gani? Kila siku taarifa zinatolewa, husikii!!

Kuna mkopo utawala wa awamu ya 5 ilichukua toka Barclays Bank wenye riba ya 8% (linganisha na mikopo ambayo huwa inatolewa na mashirika ya fedha kama WB yenye riba ya 1 - 3%).
 
Hebu nipe mfano wa kazi unayohisi italeta mzunguko wa pesa au unakaza fangasi na ukoma kuandika kitu usicho na uelewa nacho.


😂😂😂 Mtaani kapige kazi
kwa sasa biashara nyingi zinafunguliwa - ajira zipo kwa madereva, wabeba mizigo, wahasibu, mameneja, n.k. hao wanaoajiriwa wanaingiza pesa mtaani kwa kuwa wameongezewa nguvu ya kufanya manunuzi kwa mishahara, wataenda kununua nguo mitumbani, watalala kwenye gesti wawapo safari za kikazi, watanunua hardware za kujenga nyumba zao, n.k.

ni kinyume na awamu iliyopita biashara nyingi sana zilikuwa zinafungwa na watu kupoteza ajira
 
Mfumuko wa bei unafanya pesa ikose thamani hata kama una furushi la pesa, linaweza liwa lote na usijue limekwenda wapi..
Ulidanganywa na nani? Kiuchumi mfumuko wa bei wa 6-10% ndio unakuza uchumi.

Wa zaidi ya hapo ni maumivu na ndio maana unaona Tanzania uchumi unapaa
 
Sawa zitto kabwe kwa hiyo hizo hela zipo kwa sasa sio .kama ni hivyo mbona kama tupo jahanaam vile
 

Hahah eti pesa ya bure, kweli aliyesema Afrika tuna low IQ below average hakukosea, Dunia hii kuna kitu kama pesa ya bure? Inatokea wapi hiyo pesa ya bure? Inaanguka chini ya mti au? BTW average IQ TZ 70 vs rest of the World > 85, …
 

Watu wanaangalia situation on the ground ndiyo inamata na siyo majedwali ya namba, Wakenya wanaita vitu kwa ground ndiyo inayomata, watu wanaumia, Waislamu na Wakristo wote wanateseka na bei ya vyakula na kupanda kwa gharama ya maisha kupanda kwa ujumla na wala siyo swala la Magufuli vs Samia or whatever you call it ni swala la maisha ya watu sasa hivi na leo hii watu wanaumia na haijalishi mtatukana vipi lkn situation on the ground iko vingine, watu wanashindwa kulisha familia zao, maisha hayaeleweki hawajui kesho yao, shuleni
no hope watoto wanafeli Mitihani hakuna mtu anajali, future iko wapi? Hao watoto waliopata sifuri wanaenda wapi?
 
 
Maneno yote haya ni sababu ya umaskini tu. Amini ya kwamba ungekua tajiri usingeandika kilio hiki Cha uchungu. Tafuta pesa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…