wachumi wetu mko wapi?? kwanini kuna mgawanyiko mbovu wa rasilimali namna hii kwa taifa??

wachumi wetu mko wapi?? kwanini kuna mgawanyiko mbovu wa rasilimali namna hii kwa taifa??

Down To Earth

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
21,940
Reaction score
16,643
nimepakumbuka sana kwetu, nyumbani kwa baba na mama, where i was born twenty something years ago..

niko kwa muda kwa ajili ya salam za hapa na pale,

ndugu zangu, maisha ya raia wenzetu huku vijijini si mazuri hata kidogo.. ifikie kipindi tuwe tunawakumbuka na wao, hata kama hawana elimu, hawana uwezo wa kukununulia beer na kukutoa company za hapa na pale, tuwakumbuke tafadhali!

mpaka sasa, taarifa nilizonazo ni kwamba, kijiji hiki kimekumbwa na njaa kali kwa sababu ya ukosefu wa mvua kwa muda fulani hivi ambapo ulikuwa ni msimu wa kilimo! wakati wanakijiji wakilima kwa kutegemea mvua inyeshe, mvua haikunyesha hata kidogo!!!! mazao ndio yakafa hivyoo! basi katika subiri subiri, mvua ilivyokuja tu, ilinyesha kwa kuua nafaka na mazao yote mashambani!

bei sasa ya debe moja ni Tshs elfu 15, bei ya zamani ilikuwa ni Tshs elfu saba tu kitu ambacho kinaonesha uongezekaji mkubwa sana wa bei za mazao, hii ni kutokana na ukosefu wa bidhaa hiyo, lakini ina maana serikali haioni hili suala jamani?? je, kwa watu wa kawaida wasio na kipato, wataishi vipi?

kwa upande mwingine, wakati hawa raia huku kaskazini wakiwa wanalia kwa njaa, kule mashariki, mkoa wa morogoro, mazao yako yanaozea mashambani na maghalani kwa kukosa walaji!!.. je, kwa jinsi hii unaweza sema serikali yetu inaongozwa na watu wa aina gani?.. kisa tu serikali eti imegoma mazao yasiuzwe nje...!!

viongozi jaribuni kuangalia suala la mgawanyo mwema wa rasilimali za taifa!!

taifa letu si taifa la kuwa na raia wanaolialia njaa wala kulala njaa!!

ngoreme, my home!

1002095_378898065555058_1770517630_n.jpg
 
Back
Top Bottom