Wachumi wetu wafanye kazi, sababu wanazotoa na huu ushukaji wa uchumi haviendani kabisa.

Wachumi wetu wafanye kazi, sababu wanazotoa na huu ushukaji wa uchumi haviendani kabisa.

boniuso

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2013
Posts
786
Reaction score
1,043
Wanajamvi habari zenu na poleni na majukumu ya kujenga taifa.....

Nimekuwa nikiwaza kuwa ni kweli vita vya urusi na ukrane ndio sababu tu ya kushuka kwa uchumi kiasi hiki, yaani vita ndiyo sababu ya kupanda kwa bei ya sabuni, mchele mafuta ya kupikia(yalipanda hata kabla ya uchumi na yameanza kushuka),mahindi sukari (hii ilipanda hata kabla ya vita) na materials za ujenzi. Yaani inamana hizo ndio sababu za hii vita basi na hakuna kingine ???

Yaani tuseme hatuna viongozi au wachumi wabobevu wanaoweza kufanikisha hili kwa kutoa njia mbadala kwa serikari na wananchi wajue nin tufanye ili kama taifa pamoja na uchumi wa mtu mmoja mmoja uweze kuwa angalau una hauweni???

Nataka tujiulize swali hili kwa mapana zaid ya kuwa hii vita ikiisha vitu vyote vitashuka bei ?? Hebu tazama hapa sabuni kipande ilikuw 500 saizi 800-900 hapa ni vita tuu au kwa vita hii kuna watu wanajipenyeza na kupata faida kubwa maradufu???

Upandaji wa hovyo wa bidhaa muhimu kama mafuta, chakula na madawa mengine ya binadam, wanyama na kilimo hivi haviwez kuwa sehemu za siasa za watu, hapa panahitaji viongozi imara na wazarendo tuu kuweza kupigania hili. Lakin kwa hawa viongozi tunawachagua sababu ya mihemuko yetu kuna mahala tunakosea.

Labda niseme mfano mdogo tuu, swala mafuta kupanda bei ni kweli na yamesababisha hata nauli kupanda bei. Lakin huo uwiano wa nauli uwe sawa huwezi kutoka chunya mjin mpka mbeya mjin kwa elfu 4 km 78 alafu utoke makongorosi kwenda chunyamjin km 38 nauli ikawa elfu 3 na barabara zote ni kiwango cha lami. Najaribu kuwaza kama hili linatokea na hakuna kiongozi anaweza lisemea je kuna mangap kama haya yanatokea na hatuna viongozi wanayasemea?????

Rai yangu: kwanzan kabisa ni viongozi tulionao wajipambanue na waone fahali kuhudumia raia wao kwa kiwango kilichotukuka. Waone ugumu wa maisha tulionao hata wao wanachagiza kwa sera wanazopitisha bungeni bila ya kuwa na tathimin ya kina.

Pili kuwe na elimu nzuri kwa raia wapewe elimu ya kutosha kuhusu vipindi kama hivi vya mdololo wa uchumi, waambiwe ukweli sio kusema uchumi umepanda na wakati mifukoni kwao hawana kitu. Waambiwe bajeti ya mwaka huu ni trilio 40+ waone kuubwa wakazan kuwa uchumi umekuwa kumbe hapana bajet ni kubwa kwakuw maisha yamepanda sana. Piah waelezwe nin kifanyike ili waeze kuvumilia kwa kipimdi hiki, mfano waambiwe nin wafanye, biashara gan nzuri kwao, fursa za biashara zitazoendana na kipindi hiki dunia inayopitia maana huwa tunaambiwa kila tatizo huja na fursa zake BASI WATUPE FURSA ZA HII VITA marekan inasemekana ipo pale kiuchumi sababu yenyewe haikupigana vita ya dunia bali iliuza silaha na sisi tuambiwe nin tufanye kunufaika na hii vita.

Tatu kwa wananchi tujifunze kuchagua viongozi wanaoweza kutuvusha, au kushikamana na sisi kwa kila kipindi ama viongozi wataosikiliza nin tunasema ili tuunganishe nguvu zetu pamoja na kuendelea mbele, sio viongozi wataotaka kutunga sheria za kuwalinda wao kama watukufu madarakani hata wakikosea wawe na kinga kubwa huku sisi tukiumizwa na hizo sheria.

Nne, sio lazima kilajambo ifanye serikari kama kuna mahala hawawezi waite wasomi wabobebu au wafanyabiashara wakubwa , mashirika na watu binafsi wenye uwezo wakutoa ushauri juu ya nini kama taifa tunaweza kufanya ili majanga kama haya yasijekutuumiza tena au njia mbadala za haraka kunusuru taifa kwa sasa.

Kwa leo niseme ni mengi yakupendekeza, ila hayo machache yaweze tuu kuonesha ni kwa jinsi gani kama raia tunaumizwa na hali hii ya uchumi, tunajuwa mnafanya kazi sana viongozi ila bado jitihada zenu hazijaweza kutoa matokea chanya ya moja kwa moja kwetu na ndiomana tunatoa mapendekezo yetu mtusaidie. Mnaweza bana matumizi hata kwa kupunguza mishahara yenu piah maana vyeo mlivyonavyo ni vya kutumikia wananchi tena kwa kutuomba tuwape ili mtutumikie wala nyie sio madaktari bingwa au walimu au wanasheria au manesi wala sio wataalamu wa mambo ya sayansi wala sio wafanyabiashara wakubwa hivyo tuseme kuwa nyie ni wachache sana kuliko watu wanaoumiza na maamuzi yenu mnayoyafanya. Ahsate


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom