Wachungaji wanapaswa kupatiwa elimu ya afya na usalama ili kutohatarisha maisha ya raia

Wachungaji wanapaswa kupatiwa elimu ya afya na usalama ili kutohatarisha maisha ya raia

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
5,628
Reaction score
6,411
Muono wa Dunia kwenye Afya na usalama tumepewa jina "SUFURI" kwa maana ya kwamba kupunguza vifo, magonjwa na ajali kufikia asilimia sufuri.

Afya na usalama mahali pa kazi ni jambo la muhimu sana ili kuongeza ufanisi, uzalishaji na ubora wa kazi na hili ni lengo mojawapo kwenye Malengo endelevu ya Dunia kufikia mwaka 2030.

Serikali,asahi aa kiraia na watu binafsi huu ni wakati wa kupaza sauti kupunguza vifo vinavyotokea Nathalie pa kazi kwa kutoa elimu,kupanua wigo wa huduma za usalama na afya mahali pa kazi na kuongeza wataalamu wa Afya na Usalama mahali pa kazi.

Kulingana na Sera ya Afya na usalama mahali pa kazi ya mwaka 2009 ulinzi wa Aya na usalama mahali pa kazi siyo jukumu la Serikali peke yake ila linahitaji ushirikiano mkubwa sana wa Wananchi.

Hii tabia ya kulaumu vyombo vya Serikali itapungua sana endapo raia tutatambua umuhimu na jukumu letu katika kushiriki katika masuala ya afya na usalama wetu mahali pa kazi.

Unaweza ukisikia oooh...fire walichelewa...oooh watu wa usalama hawakuwepo kabisa "hiii Serikali hii hovyo kabisa"lakini jiulize wewe umeshiriki vipi kuhakikisha usalama na afya vinazingatiwa?

Maoni yangu:Wachungaji wote wapatiwe elimu wezeshi juu ya Afya na usalama mahali pa kazi "Occupational health and safety" na wao wawawezeshe wasaidizi wao kutambua na kutekeleza masuala ya Afya na usalama kwenye kazi zao mfano maombezi na mikutano yao (ya ndani au ya nje).

Pole sana Mchungaji Mwamposa sasa unapaswa kufahamu hili wajulishe wasaidizi wako na pia watumishi wengine wanaifanya kazi ya ainahiyo au inayofanana na hiyo.

Hosea 4:6 Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa.
 
Bora useme sio wanaua watu kijinga na mafuta yao
 
Back
Top Bottom