Wadada, Mkisalimiwa Jibuni Salaam, Sio Kila Salaam Ina Ubaya Ndani Yake.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Watu mmevurugwa
 
Ulikosea kwa kutokumpa funzo! Ilitakiwa umwambie mlinzi amuachie apite hapo angejisikia vibaya zaidi na angejiona mwenye hatia ikawa funzo kwake siku nyengine.

Tortured psychologically.
 
Ubaya unalipwa kwa wema

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 

Aisee ni kweli kiongozi utakuta wanaleta dharau halafu baadae wanajikuta wamekwama hata pa kutokea hawana, ndio utaona wanavyotafuta huruma.

Ni shida sana kwa kweli...!
 
Sasa kwa nini wahusishe salaam na nia ya ngono...? Kwani salaam imekaa ki-ngono ngono mkuu...?
Nakumbuka mwaka Jana niliwahi msalimia mda mmoja njiani 'mambo dada angu' matokeo yake akanifyonya!! Halafu akanambia, "kawazoee hao hao Malaya uliowazoea"
Nikabaki najiuliza, kosa langu hapo ni lipi, Kuna mama mmoja alikuwa ni rafiki yake mama yangu, alikuja nyumbani, nikatambulishwa pale, yule mama akanambia "kama utaweza naomba nikupeleke nyumbani ukawe unanifundishia mwanangu"
Kweli, siku ya kwanza nimefika nikakakuta kavulana ka darasa la sita nikakafundisha, siku iliyofuata wakati namfundisha yule mtoto, yule mdada akaingia ndani, kumbe ni dada wa huyo mwanafunzi ninayemfundisha, mama yake akanitambulisha kwake!! Hiyo aibu iliyomjaa siku iyo bhana!! Nyie acheni tu!! Na Kwa hasira nilizonazo sikuwahi kuongea nae mpaka siku namaliza huo mkataba!! Ingawaje alikuwa ananipa salamu, ila namnyamazia tu!!
 
Mawazo ya mtu husadifu kile akisemacho au kukiandika, anyway nimekuelewa uwe na mchana mwema.
Nilichoandika sio mawazo,ni kitu kipo...mimi ni wa kike,nina marafiki wa kike wenye hizo tabia na wananipa hiyo sababu

Ninae rafiki hakubali salamu ya mwanaume asiye na gari
Kwake yeye mwanaume mwenye gari ndio mwenye haki ya kuongea nae
 

Sure brother ni bora mara kumi tena, actually huwa nikimsalimia mtu mara moja hata kama tunaishia mtaa mmoja, asipoitikia tu basi hatakaa asikie sauti yangu hata siku 1.

Kuna wengine unakuta wanaonesha dharau at the same time unamkuta njiani au kituoni kasimama then hata lift huwezi kumpa, kiukweli huwa wanajikosesha vingi sana bila ya wenyewe kujijua mkuu.
 
Nilichoandika sio mawazo,ni kitu kipo...mimi ni wa kike,nina marafiki wa kike wenye hizo tabia na wananipa hiyo sababu

Ninae rafiki hakubali salamu ya mwanaume asiye na gari
Kwake yeye mwanaume mwenye gari ndio mwenye haki ya kuongea nae
Uyo rafiki yako ni mshamba sana ..unaweza kua msomi lakini still ukawa na ushamba
 

You nailed it kiongozi...!

Watu wana dharau za ajabu sana bila ya kujua huyo anayekusalimia anaweza akakusaidia kwa njia moja au nyingine.
 
Ni mwehu pekee ana kataa salamu

Thanks Nuzulati mi nafkiri hii pia inachangiwa na malezi huko walipolelewa walipewa malezi ya hovyo utakuta.

Coz ukishapewa malezi yalo mazuri toka udogoni unakua ukiwa na tabia njema kwa yeyote utakayekutana nae, ila kama malezi ni ya hovyo basi hata tabia nayo inakuwa ni ya hovyo kabisa.
 
Nilichoandika sio mawazo,ni kitu kipo...mimi ni wa kike,nina marafiki wa kike wenye hizo tabia na wananipa hiyo sababu

Ninae rafiki hakubali salamu ya mwanaume asiye na gari
Kwake yeye mwanaume mwenye gari ndio mwenye haki ya kuongea nae
Huyo rafiki yako ana dalili mojawapo za ugonjwa wa akili. Mpelekeni kwa mtaalamu wa magonjwa ya akili kabla hamjachelewa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…