Uswahilini haya ndo matatizo yenyewe,
Watu wenye Soni na haya Kama sisi, ktk mazingira haya tunajikuta katika wakati mgumu hivi.
Nijitolee mfano,,
Kipindi hicho nina girlfriend,
Nikiwa ndani pekeangu mlangoni kwangu panakua shwari kabisa,
Tatizo ni pale akija yule dada,
Yaani nikifunga mlango tu,
Ndipo nao hujisogeza mlangoni kwangu, Sasa hapo wataanza kufumua na kisukana nywele,
Watabeba majiko yao ya mkaa na kuanza kupika hapo kiasi kwamba hata baada ya kukonga nyoyo nikitoka kuangalia so, haiwezekani maana wapishi na wasusi wameegemea mlango wangu.
Dah uswahilini Kuna uswahili..