Wadada mtuelewe

Wadada mtuelewe

Foxhound

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2013
Posts
28,710
Reaction score
76,243
Salaam wapendwa. Moja kwa moja kwenye mada.

Wadada mtuelewe wanaume, sio kama tunapenda kuchepuka au kuwa na wanawake wengi bali wengi wenu siku hizi mnatufanya tuchepuke au kuwa na wanawake wengi kwa sababu zifuatazo:-

1. Mahaba (Romance)
Hamjui kumpeti peti mwanaume kama iliyokuwa kwa mabibi zetu zamani. Mmekosa mahaba kiasi kwamba mwanamke unaongea na mwanaume kama unaongea na adui au mdai wako, wakati wa kulala ndio usiseme mabibi zetu walikuwa wanawaimbia mababu zetu taarab laini, mashairi au hata nyimbo nyingine za taratibu, nyie mnalala huku mnawhatsapuka tu.

2. Mnasahau kuwa mwanaume ndio kiongozi/kichwa cha familia, kiasi kwamba nyie ndio mnataka muwe waamuzi au michangi yenu ndio ichukuliwe kama maamuzi sahihi, wengine bila kupima uzito wa jambo analochangia unakuta tayari yeye ndio kushakuwa muamuzi hadi kupelekea wanaume kuonekana aidha wamerogwa au hawako sawa kwa ndugu zao, huwa tunasikia sana hizi kauli "huyu sio bure itakuwa amerogwa na mkewe", maana kuna wengine hadi kufikia kuwafukuza ndugu na jamaa kwa ushauri wa wake zao.

3. Ubunifu sifuri (Zero creativity)
Hata kama huna hisia na mumeo bali walau buni hisia za kujifanya unafeel kile mnachofanya kwenye sita kwa sita, maana huku tulikofikia hali ni mbaya, mwanamke unado na mumeo mara umeshika simu mara unamuuliza ushamaliza mara ooh! mi nimechoka nataka nilale mara bado tu. Mnajididimiza wenyewe we unadhani mwanaume kama huyo akitoka nje akipata kidada cha mtaa wa mbali au hata jirani ambacho kwenye sita kwa sita kinajituma, mara kifo cha mende, mara paka mgonjwa, mara nyigu mzee, mara popo kanyea mbingu, mara dogstyle mara missionary kwa akili zako unafikiri mwanaume kama huyo atakaacha hako kabinti?

4. Hamna shukurani
Mwanaume amerejea toka safari amekuletea vijizawadi walau viwili vitatu, kweli unashindwa kumshukuru huyo mwanaume, na wengine hufikia hadi kuonesha dharau "Vijizawadi vyenyewe ndio hivi" bila kujali kuwa unamvunja moyo huyo alokuletea hizo zawadi. Muelewe kuwa mwanaume huyo akipata kidada mtaani ambacho kinapokea kila kinachopewa basi huyo mwanaume anaweza kuganda kwa hicho kidada, anaweza akakuletea wewe zawadi na ukionesha dharau anapelekewa huyo kadada.

Wadada mtuelewe, sina nia mbaya nanyi ila nataka walau mpate elimu ambayo itawasaidia, wanaume tunahitaji mahaba, tunahitaji kupewa ushauri mzuri wenye kujenga na sio kubumoa, tunahitaji kufanyiwa ubunifu, tunahitaji kuonekana kama viongozi wa familia, tunahitaji kupewa shukrani pale inapobidi.
Najua kuna mengi nanyi mnayo, nakaribisha majadiliano sio povu!
[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Lakini na nyie pia naomba mtuelewe.


Kuna baadhi ya wanaume hawajui kuwajari wapenzi wao yani hawawapi muda wa kukaa nao wakabadilishana mawazo,Mwanamke mwenye mapenzi ya kweri anahitaji muda wako zaidi na hawezi kukufanyia hayo uliyoyasema,heshima atakupa ,atakujali atakusikiliza na sio vinginevyo
 
Lakini na nyie pia naomba mtuelewe.


Kuna baadhi ya wanaume hawajui kuwajari wapenzi wao yani hawawapi muda wa kukaa nao wakabadilishana mawazo,Mwanamke mwenye mapenzi ya kweri anahitaji muda wako zaidi na hawezi kukufanyia hayo uliyoyasema,heshima atakupa ,atakujali atakusikiliza na sio vinginevyo
Ssafi sana, napenda kujadiliana na mtu mwenye uelewa kama wewe, sasa je kama mwanaume hayo yote anayafanya lakini hakuna mwamko kwa upande wa mwanamke unashauri afanyeje ili waende sawa?
 
Mkiahidi zawadi mkuje nazo basi...

Nakudai zawadi zangu mimi
[emoji16]PM umefunga bana[emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2445][emoji2445][emoji2445]
 
Lakini na nyie pia naomba mtuelewe.


Kuna baadhi ya wanaume hawajui kuwajari wapenzi wao yani hawawapi muda wa kukaa nao wakabadilishana mawazo,Mwanamke mwenye mapenzi ya kweri anahitaji muda wako zaidi na hawezi kukufanyia hayo uliyoyasema,heshima atakupa ,atakujali atakusikiliza na sio vinginevyo
Ukipewa kipande kimoja cha dhahabu na kipande kimoja cha jiwe unafikiri ni kipande kipi kitatawala akili yako??

Kama ME wako hakufikirii jua ashakuona kama jiwe, yani upoupo tu[emoji1][emoji1][emoji1] KE lazima umfanye ME akuone kama dhahabu
 
unajisumbua mkuu yaani mkeo aanze kukuimbia taarab halafu whatsapp amuachie nani?

nafkiri utandawazi ndo umeharibu nao wameruhusu uwaingie.
unakuta hawezi kukaa 30 min bila cm yake
 
Mkiahidi zawadi mkuje nazo basi...

Nakudai zawadi zangu mimi
Ahadi ziwe pande zote mbili
IMG_20190802_130737.jpeg
 
Back
Top Bottom