black abdu
Senior Member
- Dec 2, 2022
- 156
- 212
Kuna hii kadhia ya kwenye daladala zetu, inanikera sana, ya abiria kusimama mistari miwili wakielekezana migongo. Makondakta wana ujuzi wa kupanga abiria, huoni hata nafasi imeachwa.
Msongamano huu upo pia kwenye Mabasi yetu ya Mwendokasi, ingawa kule utaratibu si kama we kwenye daladala. Ukweli huu utaratibu huwa unanikwaza, mara nyingi huwa najiweka nyuma ya dereva, hata kondakta akisema rudi nyuma sikubali, naacha nafasi ya watu kupita.
Wengine huwa nawaona wapo sawa tu, hawajali, wameshakubaliana na uhalisia wa hali. Mimi huwa nakwazika sana ile kuwekeana makalio hasa wanaume kwa wanaume au wanaume kwa wanawake.
Nawaona wanaojiachia zaidi ni wanawake, yaani ni kama hawana habari na huko nyuma, mtu kasimama hajigusi, ukipita uji-tune mwenyewe. Mwanaume mwingine nae kawekeana makalio na mwanamke, katulia tulii, sijui nini huwa kunaendelea akilini mwao wakati huo.
Binafsi namueheshimu sana Mwanamke, thamani ya maungo yake ni kubwa, haistahili kuguswaguswa hovyo. Sawa, ndio uhalisia wa hali, basi angalao wangekuwa hata wanajaribu kujihepesha, lakini hakuna. Siku moja nimekaa, mwanamke mmoja anashuka, kainama kuchukua mzigo wake, kalio lote kaniwekea begani! Heee! Aibu naiona mimi.
Kuna watu wana maradhi, hawawezi kuhimili kugusana na ndio zile hadithi unasikia mtu kachafuliwa, inakuwa gumbo. Au njemba mwengine kawekea "bogi" anajua dada watu anamtaka, anaanza kuji-tune na yeye, baadae mdada anahamaki inakuwa fedheha.
Heshima ya dada daladalani aitunze nani?
Wasalaam!