Wadada wa kazi na kupasua vyombo

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
27,031
Reaction score
49,928
Jamani hawa wasaidizi wetu wa ndani tunawapenda na tunawajali sana.yale maisha ya wasichana wa ndani kulazwa chini,kunyimwa msosi, kupigwa ,kutothaminiwa kwa kweli siku hizi yamepitwa na wakati.sasa hivi ukienda kwa mtu hata kujua beki tatu ni yupi inakuwa shida maana tumewapendezesha hadi basi. hata wababa ndani hawajui mke ni yupi au beki tatu ni yupi kote mnapakua tu

Ila jamani kuna shida moja naiona hata nimejadili na wamama wenzangu .unajipausha maka mzima kukopa vicoba ili ununue vyombo vizuri ila jamani jamani wanavipasua hao .sijui kuna pepo ama nini.

Mimi nilikaa mwaka mzima bila dada sijawai kupasua hata chombo kimoja ila dada kaja miezi mitatu naona sasa bila kupasua kitu hapumui.

Tufanyeje jamani maana ukikata mshahara unaonekana mbaya.ukifukuza a naekuja nae kama anakuja na nyundo yake rohoni
 
Ukiona ameendelea kupasua fanya kama umemkata mshahara. Lakini hela yake itunze sehem siku akita kwenda mpe hela yake. Kama kweli ni mtaftaji atabadirika tu
 
Vyombo vyako special ambavyo vina umuhimu kwako weka mbali aisee.

Utakuja kuumbuka kwenye special event huna chombo cha maana. Cutlery zote zimesuguliwa kwa steel wire, vikombe vyote na sahani vina ufa, chupa ya chai ndo unagundua haina hata yai. Lilishatagwa
 
ahaaaa halafu kaipanga kabatini hana hata habare.
 
kwaiyo unataka turudi enzi za vyombo vya wageni sio.tutumie plastic vyombo vizuri visubirie siku maalum? siku maalum ni ipi sasa jamani maisha yenyewe mafupi?
 
Ukiona ameendelea kupasua fanya kama umemkata mshahara. Lakini hela yake itunze sehem siku akita kwenda mpe hela yake. Kama kweli ni mtaftaji atabadirika tu
huruma mwenzangu .
 
kwaiyo unataka turudi enzi za vyombo vya wageni sio.tutumie plastic vyombo vizuri visubirie siku maalum? siku maalum ni ipi sasa jamani maisha yenyewe mafupi?
Hapana. Nisome vizuri. Vyenye umuhimu kwako. Mimi nyumbani kwangu situmii plastics na watoto hawatumii plastics pia.

Wanatumia vyombo vizuri tu vya udongo. Sasa na wewe weka vyombo vizuri mezani but save the best for last.
 
Mara nyingi huwa ni bahati mbaya na sababu kubwa ni vyombo kuteleza sababu ya sabuni,kulundika vyombo bila kuosha na wakati wa kuosha anachanganya vyombo vyooote sehemu moja ndo aoshe.

Mpe maelekezo, asubuhi baada ya chai aoshe vikombe afute na apange kabatini, mchana hivyo hivyo ila aanze na glass kwanza ahakikishe amezifuta na kuweka panapostahili. Aendeleee na sahani au bakuli!!!! Jioni hivyo hivyo!!!! Lakini akiacha vikombe,vyombo vya mchana aoshe na vya asubuhi lazima atavunja!!!!

Akizoea hivyo haitakuwa rahisi kuvunja tena kuvunja.

Mie huwa naosha vyombo vyangu jioni na weekend asubuhi na jioni!!! Ila dada niliyenaye yuko makini sana
 
Hapana. Nisome vizuri. Vyenye umuhimu kwako. Mimi nyumbani kwangu situmii plastics na watoto hawatumii plastics pia.

Wanatumia vyombo vizuri tu vya udongo. Sasa na wewe weka vyombo vizuri mezani but save the best for last.
yaani hata ukitoa vichache si anapasua tu.wewe unafanyeje vyombo vyako visipasuliwe? tuanzie hapo kwanza
 
yaani sakayo wala hatuachi vyombo vikawa vingi ila bado tu vinapasuliwa labda kuna pepo home .
 
Maadui zako wa JF wanadai eti unatafuta kik kwa pikipiki!![emoji30][emoji30][emoji30]
 
yaani sakayo wala hatuachi vyombo vikawa vingi ila bado tu vinapasuliwa labda kuna pepo home .
Ni kila siku au??? Mwambie asiwe anaweka kwa kutusha kwenye mabeseni wakati wa kuosha!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…